Home Kitaifa Tundaman awaweka nje Ajib na Mahadhi tayari kwa hatua ya 16...

Tundaman awaweka nje Ajib na Mahadhi tayari kwa hatua ya 16 bora

11298
0
SHARE

Michuano ya Ndondo Cup 2018 imeendelea hii leo kwa michezo miwili kupigwa, kule Bandari Goroka Fc waliambulia kipigo cha bao 3-1 mbele ya Makuburi huku Kinesi New Life wakiipiga Goms bao 1-0.

New Life pamoja na kumaliza wakiwa pungufu baada ya mfungaji wa bao lao kupewa kadi nyekundu lakini waliibuka na alama 3 zilifowanya kufikisha alama 4.

Baada ya mchezo huo Dauda Tv ilifanikiwa kupiga story na moja ya viongozi wakuu wa New Life Fc ambaye pia ni mmoja mwanamuziki wa Bongo Flava Tunda Man.

Tunda anasema pamoja na changamoto ambazo walikumbana nazo hii leo lakini anaamini vijana wake wako vizuri sana na wana timu nzuri sana ndio maana hadi sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Tunda amesema pamoja na ukweli kwamba timu yao haina majina makubwa kama timu nyingine lakini wako tayari, na si tu kwamba hawana majina makubwa ila wapo wengi amewapumzisha kwa ajili ya hatua ya 16 bora.

Katika mchezo wa leo Tunda aliandamana na nyota wawili wa klabu ya Yanga Juma Mahadhi na Ibrahim Ajib akisisitiza kwamba wakati ukifika atawaanzisha wachezaji hao na wengine alionao, hii hapa full interview ya Tundaman nimekuwekea You Tube.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here