Home World Cup RUS2018: Xhaka aharibu hali ya hewa, Brazil kutegwa na Serbia

RUS2018: Xhaka aharibu hali ya hewa, Brazil kutegwa na Serbia

11250
0
SHARE

SERBIA 1-2 USWISI

Mechi ilivyokuwa:

Serbia walianza kipindi cha kwanza kwa haraka wakitaka pointi tatu, ili wajihakikishie kufuzu kabsa.Alexander Mitrovic aliipatia Serbia goli la kuongoza dakika ya 5.Serbia ndio walioonekana kuutawala mchezo kuliko Uswisi, na hata Uswisi ni kama hawakuwa mchezoni baada ya goli lile sababu goli la mapema huwa linachanganya.

Serbia walijitahidi kutengeneza nafasi kipindi cha kwanza tatzo lilikuwa kwenye kumalizia, Wamekosa baadhi ya magoli na baadae kabla ya kipindi cha kwanza Mitrovic kidogo aipe Serbia goli la 2, na wangeenda mapumziko wakiwa wanaongoza 2-0.

Dusco Tosic alikosa goli baada ya kupokea pass mpira wa kona uliopigwa na Dusan Tadic, hivyo Serbia walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa wametengeneza nafasi chache, nadhani walijilaumu pia kwa kukosa nafasi zao.Umakini ndo ilikuwa tatzo pamoja na kwamba Uswisi walijitahid kuzuia ila walioonekana kuwa bora kipindi cha kwanza kiliko Uswisi.

Mladen Krstjic, kocha wa Serbia huyu ni kama aliona timu iko kwenye nafasi nzuri baada ya kwenda mapumziko ikiwa inaongoza na kujipa matumaini na pia hata ile nguvu ya kupambana kwa Serbia niliona kama imeshuka baada ya kipindi cha pili kuanza. Naamin aliwaelekeza wachezaji wakati wa mapumziko na kazi ilibaki kwa wachezaji kutekeleza lakin hawakutengeneza nafasi kama walivyofanya kipindi cha pili.

Vladmir Petkovic, kocha huyu wa Uswisi naamin kabsa ndo ameshinda kimbinu zaidi, maana aliona timu yake imemaliza kipindi cha kwanza ikiwa nyuma na ikumbukwe Uswisi walikuwa tayari wana pointi moja baada ya kutoa suluhu dhidi ya Brazil. Hivyo kocha alichofanya ni kuwambia kwamba tayari Serbia wana pointi 6 muda huu, ndomaana walikuwa na hali kujiamini kipindi cha kwanza.

Xhaka na Xhaqir na wachezaji wenzao wa Uswisi walianza kipindi cha pili wakiwa hawaonyeshi kuchoka na walianza vizuri sana. Walitaka ushindi mno maana kupoteza ingekuwa mbaya zaid, walijaribu kupiga mashuti mengi na kushambulia kwa kasi zaidi na hawakukata tamaa, walipambana mpaka wapate matokeo. Nawataja Xhaka na Shaqir sana maana ndo wameifanya mechi iwe nzuri na ya kuvutia mpaka huwa nataman mechi zote ziwe kama hivi.

Kutoka nyuma na kushinda haikuwa kazi rahisi. Katika mashindano haya ya kombe la dunia mwaka huu, Uswisi ndo imekuwa timu ya kwanza kutoka nyuma na kuibuka na ushindi.Kilichoisaidia Uswisi wana mchezaji (Shaqir) ambaye anaonekana ni (game changer) maana yake anaweza kubadilisha matokeo na anaweza kuwa man of the match huyu au nyota wa mchezo. Kingine kilichonifurahisha ni kwamba haya mashindano kiukweli yanavutia mwaka huu, yan hatujashuhudia mechi inaisha bila kufungana.Timu zote zimefungana na hii ndo imefanya binafsi nifurahie mashindano ya mwaka huu.

Kazi nzuri kwa Uswisi, nguvu yao ilikuwa ya hali ya juu sana na tayari wamejirahisishia kufuzu maana tayari wana pointi sawa na Brazil, point nne. Mechi yao ya mwisho wanacheza na Costa Rica ambao tayari wanaonekana tayari wameshaaga mashindano maana mpaka sasa hawana pointi hata moja..

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here