Home World Cup RUS2018: Messi amepata tabu sana, lakini tusimdhihaki ili kumkweza Ronaldo

RUS2018: Messi amepata tabu sana, lakini tusimdhihaki ili kumkweza Ronaldo

11501
0
SHARE

Hata uwe mzuri vipi, kama wewe ni binadamu kuna wakati mambo yako lazima yakwame. Kuna wakati inabidi tukubali kwamba mipango ya wanadamu ina pande mbili za lazima (Kwenda sawa au kwenda Mrama). Kuna watu wanamdhihaki Messi.

Wazungu wanasema sometimes shit happens. Hilo halina kipingamizi. Waargentine wanamuona kama Messi ni malaika. Yaani kila jambo likienda mrama kwao wanaammbwagia mzigo wote Messi.

Ukiachana na waargentine kuna wengine wanadai Messi ana timu bora zaidi.

Nimejiuliza hiyo timu bora kwa Argentine ni ipi? Mwisho wa siku wataishia kutaja washambuliaji pekee yao. Kiungo gani bora wa kuimarisha la dimba la kati?

Msimu huu Messi nyuma yake wapo babu Mascherano ambaye hata namba Barcelona msimu huu alipata namba kwa rehema za mola akisaidiana na Mzee Enzo Perez mwenye miaka 32. Hawa wote wameshapitwa na wakati na ndip waliotumwa kumwinua Messi.

Argentine ina kikosi kidogo mno tofauti na mnavyodhania. Yaani benchi lao huwezi kuligeukia mara mbili kutafuta mchezaji mkubwa utaishia kumkuta Higuain na Dybala aliyesuswa pamoja na Miguu ya biskuti ya Rojo ambaye kama ningekuwa kocha wa timu yao ya taifa nisingemwita.

Angalau wanaubora kwenye safu ya ushambuliaji pekee. Mtu anaweza kusema kama shida ni safu ya ulinzi na Viungo, je kwanini akina Messi wameshindwa kupata bao! Jibu ni moja tu, Hapo awali nimesema sometimes shit happens.

Niwarudishe mwaka 2002. Ufaransa walikwenda Korea wakiwa na kikosi bora mara 10000 ya hiki cha ufaransa. Walikwenda na kiungo bora wa Madrid Makelele, Walikuwa na Kiungo bora duniani Zinedine Zidane akisaidiwa na Patrick Viera, Nyuma walikiwepo vichaa wa Bayern Willy Sagnol na Lizarazu, walikuwa na Beki bora wa Juventus Lilian Thuram. Mbele walikuwa Mshambuliaji mwenye kasi zaidi katika kizazi cha wafaransa Thiery Henry, alisaidiwa na Cisse na mshambuliaji maridhawa wa Juventus David Trazguet na Sylvian Wiltod wa Arsenal. Samahani nimemsahau na Emmanuel Petit alishika dimba la kati.

Huwezi kuamini kikosi hiki kilifunga mabao matatu tu na kuruhusu mabao matatu.

Sitoacha kuwambia kwamba Sometimes shit happens. Hii ni kawaida kabisa hii katika soka mambo hayaendi. Sio Argentine tu wanafanya vibaya mataifa mengi tu yanazingua. Ujerumani 2002 wakiwa na Oliver khan walizingua, 2006 wakiwa na Ballack wakazingua, 2010 wakiwa na Muller wakazingua. Sio Messi tu ila sometimes shit happens.

Hispania 2014 ni mfano mwingine tosha. Huu mzigo mnaompa Messi pekee yake mnamuonea ile no timu wapo wachezani wengine ambao wanavibeba vilabu vyao kama Aguero. Kama Aguero aliokoa Man city kwenye mdomo wa Ferguson 2011 kwanini wasimlaumu na yeye? Mbona zidane aliwadhalilisha De lima na dinho na watu wakajifanya hawakuona?

Kikosi cha Jana hakikuonesha
spiriti ya timu inayohitaji matokeo ya ulazima. Kilikosa mbinu za kumiliki mpira. Watu wanalalamika sijui Icardi hayupo. Ni kwelo Icard ni mchezaji mzuri, na hatuwezi kujua kama angeitwa angeonesha nini maana kila mtu na bahati yake. Argentine ilifeli kuanzia katikati sio ubutu wa kufunga tu. Hiyo kazo ya Icard Messi na Aguero walitosha kuifanya. Icard sio kwamba ana uwezo kuwazidi wale wote waliotwa. Alifanya vizuri sana na alihitajika sana kikosini kwa kiwango chake lakini hakuwa bora kuliko waliotwa. Wachezaji wengi wa kiungo cha kati Argentine wamejichokea. Timu ilikuwa inacheza ovyo hadi Messi akaonekana mbovu sijui Icard angefanyaje.

Inawezekana kweli Icard ma Dybala walihitajika Lakini Messi na Aguero, Higuain hawa wote ni bora na wamezoeana kwa muda mrefu na wamekuwa na mafanikio. Hao wote ni bora kuliko Hao Icard na Dybala. Wamefika fainali tatu kubwa duniani kwa kipindi kifupi bila msaada wa hao walioachwa. Sawa ni kweli kila mchezaji ana nyota na bahati yake hilo haliepukiki hivyo hatuwezi kujua Icard na Dybala wangeleta ladha gani.

Kosa limwendee Sampaoli ambaye yeye anajua kwanini hao hawajaitwa.

Turudi kwenye mada yangu, kuhusu mafanikio ya Messi na Ronaldo timu ya taifa. Juzi nilisema Messi anawapa sabuni Waargentine wao wanampaka matope.

2007 Aliifungia Argentine mabao muhimu kabisa katika kombe la Copa America lakini fainali walipoteza dhidi ya Brazil. Hakucheza fainali kwa kigezo kwamba alikuwa mdogo. Ni mchezaji bora kwa taifa hilo kwa mara 11. Kama wanamuona hajitumi kwa taifa kwanini wanampa hiyo tuzo? Messi ni Mchezaji pekee wa Argentine aliyeifunga kila timu ya CONMEBOL. Hayupo mchezaji bora zaidi ya Messi huko Argentine. Hakuna mchezaji mwenye mabao mengi huko Argentine. Wala sioni mchezaji mwenye uchunu na taifa hilo. Alichokosa Messi ni upayukaji na uhamishaji mkubwa uwanjani. Sio muongeaji kabisa.

Haonekani kuwa nahodha mzuri. Amekuwa mchezaji mzuri lakini amekjwa akisshindwa kufanya majukumu mengine yeye kama. mchezaji ndani ya uwanja. Ni tofauti kidogo kwa Ronaldo. Ronaldo ni kiongozi mzuri na anajua kuwatia wenzake moyo. Messi juzi wakati wa wimbo wa taifa yeye tayari alishakata tamaa. Sio kosa lake kila mwanadamu ameumbwa tofauti.

Messi tayari ana medali 4 Ronaldo anayo 1. Achilia mbali kombe la olympic. Ronaldo amekuwa mpambanaji mzuri kwa taifa lake sana sawa tu na Messi sema watu wanajificha kwenye kivuli cha majina ya wachezaji. Tumemuona Ronaldo alivyosimama imara na kuhakikisha vilena wa Ureno wakapata ubingwa Yuro. Ni uongozi wake ndio ulioleta chachu kwa wenzake.

Sijui kwanini wanamdhihaki Messi, Kama wachezaji wenzake hawachezi kwa kijituma mnataka Messi atoke goli hadi goli akafunge? Mlitaka Messi adake? Timu imecheza hovyo kila mtu ameona.

Timu kumdumaza mchezaji bora ni kawaida sana. Sio kwamba Ronaldo hajapitia haya maisha.

2010 Ronaldo alitoka kapa kule Afrika Kusini, 2014 akatoka kapa kule Brazil watu wakasema mgonjwa.

Messi na Ronaldo wote wamepita nyakati ngumu katika mataifa yao. Wadau wanasahau kama Ronaldo ambapo alidumu kwa miezi 16 bila kufunga bao lolote kwa timu yake ya taifa akaja akafunga bao pekee michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 kwenye ushindi wa mabao 7 dhidi ya korea?

Wengine wanasahau kuwa kiwango cha Argentine kwenda kombe la dunia kilikuwa cha kusuasua tena huyo huyo Icard alikuwemo michezo minne na hakufanya lolote ila tu palionekana kukosekana kwa maelewano mazuro na wenzake. Timu ilibiddi isiburi mchezo wa mwisho kufuzu. Ronaldo nae pia mwka 2014 ilibidi apitie mlango wa uwani kufuzu kombe la dunia kwa kuifunga Sweden mabao matatu. Haya mambo yapo tu. Ni kawaida sana kwenye soka

Sio kweli kwamba Ureno 2014 ilikuwa mbovu. Mnatudamganya tu. Alikuwepo Nani wa Man United, Alikuwepo Raul Miereles aliyebeba ubingwa wa Uefa na chelsea, alikuwepo Coentrao wa Madrid, huwezi kumkataa Pepe, Ni ngumu kukataa kiwango cha Moutinho, wala hakuna mtu asiyejua uwezo wa William Carvalho. Ubora wa wachezaji sio vilabu wanavyocheza ila uwezo wao.

Brazil 2002 walibeba kombe la dunia wakiwa na wachezaji karibia 17 waliocheza ligi ya Brazil. Kwa hiyo unaweza ukawa na wachezani wenye majina makubwa kutokana vilabu wanavyocheza. Nyie hamuoni Tarkowsk wa Burnley ameachwa kachukuliwa Jones wa Man United. Mtu anaweza kuwa timu kubwa lakini akazidiwa uwezo na aloyepo timu ndogo. Hivyo Ureno sio kwamba no wabovu. Ila wachezaji wake walikuwa vilabu vya kawaida.

Wapo wanaombeza Messi kwa takwimu za mabao wakimlinganisha na Ronaldo.

🇵🇹 Ronaldo ana mabao 85 kwa taifa lake:
amefunga mabao 50 katika hatua ya kufuzu na mabao 18 katika mashindano na mabao 17 katika mechi za kirafiki.

Ronaldo ammecheza dhidi ya timu 37

🇦🇷 Messi amefunga mabao 64, Mabao 21 katika hatua ya kufuzu na mabao 13 kwenye mashindano. mabao 30 mechi za kirafiki

Mimi nadhani takwimu muhimu ni hizi za kufuzu na mashindano.

Takwimu zinaonesha kwamba Messi amepitwa mabao matano tu Ronaldo katika hatua ya Mashindano. Hatua ya kufuzu ni kweli amemzidi mabao 30.

Messi amecheza dhidi ya mataifa 28 tu unaweza kuona Ronaldo amecheza na mataifa 9.

Hatua ya kufuzu ulaya ina nafasi nyingi zaidi za kucheza tofauti na Amerika nikimaanisha michezo ni mingi. Messi amecheza michezo 126 na Ronaldo 154 zaidi ya michezo 20. Hivyo unaweza kuona kwa namna gani wote hawapishani sana na wamekuwa na umuhimu mkubwa kwa mataifa yao.

Wote naona wanapambana kila mmoja kwa uwezo wake na kwa nafasi yake. Sio kweli kwamba Messi ni mbovu kwa taifa lake bado ameonesha uwezo mkubwa sana na amepambana kwa kiasi chake.

Messi na Ronaldo wote wamepambania mataifa yao kwa juhudi na nguvu zao. na wanahitaji pongezi.

Sio lazima ukubaliane na mimi ila mimi naona wote wanajituma na wote wamekumbana na hali ngumu. Makala imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here