Home World Cup RUS2018: Pogba mzigoni tena leo

RUS2018: Pogba mzigoni tena leo

8862
0
SHARE

Kuelekea kwenye mechi nyingne ya kundi C, kati ya Ufaransa na Peru ambayo itachezwa saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika mashariki katika mji wa Yekaterinburg. Hizi ni taarifa za timu

UFARANSA
Ilithibitishwa kwamba Antoine Griezman alipata jeraha la kifundo cha mguu kabla ya mchezo dhidi ya Australia na alicheza huku akiwa na maumivu, lakini haitarajiwi kuwa na tatzo jipya kwa Griezman au kwa mchezaji mwingne wa kikosi cha Ufaransa kuelekea kwenye mchezo huu.

PERU
Paolo Guerrero alianza mashindano akiwa benchi dhidi ya Denmark akihangaikia kurudi kuwa fiti.Ukiacha mshambuliaji, hakuna lingne jipya linalowahusu Peru.

Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps;Niliona timu nyingi ambazo zina magumu kama ya kwetu na matokeo sawa.” Tutaona kesho ambaye atacheza. Tatizo la Olivier, Anacheza peke yake, hayuko sawa na wengne lakin kipindi ambacho hayupo kule , tunatambua jinsi anavyotumika.Anaweza kuanza.

Kocha wa Peru Ricardo Gureca, Ni kweli tunawaheshimu Ufaransa lakini haijalishi, tunadhaniwa kuwa ni timu ndogo, ni kama tunaishi kwenye mpaka.Tunaweza kuifunga timu yoyote.Tuna vifaa vya kushinda na tunajua namna ya kujilinda wenyewe.Katika kipindi hiki, sijui kama tulikuwa kwenye kiwango kimoja kwa sehemu yoyote, kusema ukweli.Tunaendelea kuimarika na kutaka kuzoea kiwango cha juu haraka iwezekanavyo.Ila kitu muhimu ni kwamba tunabaki kwenye ukweli wetu na staili yetu, na tunaamini kwamba tunaweza kuwa wagumu kuipa shida timu yoyote, hatutawaacha Ufaransa watusukume karibu.

Kumbukumbu
Ufaransa na Peru, mechi yao ya mwisho kukutana ilikuwa ni mechi ya kirafiki mwezi wa nne, 1982.Peru ambayo inatoka bara la Amerika ya kusini ilishinda 1-0

Timu ya mwisho kutoka Amerika ya kusini kuifunga Ufaransa kwenye kombe la dunia ilikuwa Argentina mwaka 1978.

Kikosi cha Ufaransa kinachoweza kuanza: Lloris, Parvad, Varane, Umtiti, Hernandez, Kante, Pogba, Matuidi, Mbappe, Griezman, Giroud

Kikosi cha Peru kinachoweza kuanza; Gallese, Advincula, Ramos, Rodriquez, Trauco, Tapia, Yotun, Carillo, Cueva , Flores, Farfan

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here