Home World Cup RUS2018: Mganda kuwavaa Australia leo

RUS2018: Mganda kuwavaa Australia leo

9715
0
SHARE

Leo jumanne kutakuwa na mechi nyingne ya kundi C kati ya Denmark na Australia, ambayo itachezwa majira ya saa 9:00 saa za Afrika mashariki.

Zifuatazo ni taarifa za timu zote mbili.

Denmark: Andreas Christensen na Willian Kvist wote walitolewa nje baada ya kupata majeraha wakati wa ushidi dhidi ya Peru. Andreas amepona na yupo kwaajili ya kuchaguliwa kuanza mechi.Lakin Kvist inawezekana asicheze kabsa kwenye mashindano.Na Lasse Shone anatarajia kuchukua nafasi yake.

Australia: Kocha ana uchaguzi ambao ni mgumu kati ya Andreas Nabbut kuongoza safu ya ushambuliaji au kumchagua Tomi Juric, ambaye amepona baada ya kutoka kuuguza majeraha na yupo tayari kucheza.

Wanaweza pia kumuita kijana mdogo Daniel Arzani na mchezaji mkongwe Tim Cahil kuwepo kwenye ratiba ya mechi ya pili ambayo ni lazima washinde kufuatia kipigo cha 2-1 kutoka kwa Ufaransa.

Mitazamo ya wachezaji pamoja na kocha kuelekea kwenye mchezo huo.

Kocha wa Denmark Age Hereide amesema kwamba, Australia wanaonekana imara kama timu na Waaustralia mara nyingi wanajituma sana,wanapambana kwa moyo wote na wana akili sana.

Nafikiri Australia wanaonekana bora siku baada ya siku.Tangu Van Marwijk alipokuja ameonekana ni kocha mzuri na mzoefu.

Australia: Kiungo wa Australia Aaron Mooy akizungumzia mipango yao,” Tuna mbinu mbadala ya mchezo ,ambayo tumecheza. Kocha Bert na benchi lake zima la ufundi tangu walipokuja hakuna mabadiliko mengi, tunajaribu kufanya kazi yetu vizuri.

Mbinu ya mchezo ilifanya kazi dhidi ya Ufaransa, labda tunahitaji kushambulia zaidi lakin hiyo inategemea na mechi jinsi itakavyoendelea. Tunahitaji kushinda hivyo tuna matumaini tutapata nafasi chache na kuzitumia.

Unajua kwamba

Timu zote mbili zimekutana mara ya nne na timu ya Denmark imeshinda mara mbili. Kasper Schmeichel katika mechi tano za Denmark hajaruhusu goli kuingia kwenye nyavu zake.

Vikosi vinavyoweza kuanza:

Denmark- Schmeichel,Larsenz,Christensen,Kjaer,Dalsgaard,Shone,Delaney,Eriksen,Sisto,Jorgensen, Poulsen,

Australia- Ryan,Behich,Milligan,Sainsbury,Risdon,Mooy,Rogic,Jedinak,Kruse,Juric,Jeleikie

by Admila Patrick

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here