Home World Cup RUS2018: Messi kitanzini tena

RUS2018: Messi kitanzini tena

11548
0
SHARE

Leo Alhamisi, kutakuwa na mchezo wa kundi D, utakuwa na mchezo wa mwisho wa siku ya Leo. Argentina, atacheza dhidi ya Croatia, katika dimba la Novgorod Stadium. mchezo huo utapigwa majira ya saa tatu kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kocha wa Argentina, Jorge Sampaoli, anaweza kuleta mabadiliko katika kikosi chake baada ya mchezo wao wa Kwanza kupata sare ya mabao 1-1 dhidi ya Iceland.huku akitegemewa zaidi mchezaji wa klabu ya Boca Junior, Cristian Pavon, kuanza katika mchezo wa leo.

Kocha wa Argentina, Jorge Sampaoli, akiongelea tukio ambalo Lionel Messi, kukosa penalty katika mchezo wa Iceland.

“Lionel, atakiwi kubeba majukumu yote katika timu ya taifa. Tunaongelea kombe la dunia ambalo linaangaliwa na mamilion ya watu tunaweza kukosa penati katika soka. mda mwengine mpira una matokeo yake tunatakiwa tukubaliane na matokeo.

“ni mchezaji bora wa dunia na siwezi kumfananisha na mchezaji yoyote duniani.timu ikipoteza mchezo basi tumepoteza wote.

“amepata plesha kubwa baada ya kukosa penalt na pia Messi, akifunga huwa tunafurahi zaidi.

Croatia, itamkosa mshambuliaji wake Nikola Kalinic, baada ya kufukuzwa katika timu hiyo kwa kosa la utovu wa nidhamu. Mshambuliaji huyo alitakiwa aingie katika mchezo wao dhidi ya Nigeria, mnamo dakika ya 85 na kusema hawezi kuingia kwa sababu amepata maumivu ya mgongo na badae kugundulika alikuwa amedanganya.

Kocha wa Croatia, Zlatko Dalic, amesema kuwa Messi, ni moja ya mchezaji bora duniani na kumzuia itakuwa ngumu mno.

“mchezo wa leo kumzuia Messi, itakuwa ngumu ila tutahakikisha Messi, apigi pass za mazara langoni kwetu.pia Argentina, ina wachezaji wenye ubora na hachezi mwenyewe kwenye timu hiyo.

Kumbukumbu. Argentina, ameshinda michezo miwili Kati ya michezo minne, aliyokutana dhidi ya Croatia. Kushinda 2, sare 1, kupoteza 1.

Mara ya mwisho Croatia, kukutana na Argentina, Croatia, alifunga bao 1-0 fainali za Mwaka1998 , kule nchini Ufaransa.

Vikosi vinavoweza kuanza Leo.

Argentina. Caballero, Salvio, Otamendi, Rojo, Tagliafico, Mascherano, Bilgia, Pavon, Messi, Di Maria, Aguero.

Croatia. Subasic, Vrsaljko, Lovren, Vida, Strinic, Modric, Perisic, Kramaric, Rebic, Mandkuzic.

Vipi hali ya Lionel Messi

Messi anajituma sana timu yake ya taifa. Kuliko watu wengi wanavyodhani. Huwa nikiangalia mchezo wao namuangalia yeye tu. Hata hivyo hakunaa mchezaji mwingine wa Argentine wa kumuangalia. Shida kubwa wachezaji wa Argentine hawana bahati nzuri sana ya kuelewana nakimaanisha mwaka huu pekee. Watu wengi wamekuwa hawaoni mafanikio ya Messi na Argentine. Tumekuwa na kasumba ya kuamini kwamba kunyanyua makwapa peke yake bila kujua kwamba fainali zinacheza timu bora. Ndani ya miaka 6 Argentine imeingia fainali 3 licha ya kupoteza zote. Kiuhalisia hili ni taifa lenye wachezaj wenye medali tatu ndani ya miaka 6 kwa taifa lao hakuna taifa lingine kubwa lenye mafanikio haya. Messi anapambania taifa lake lakini kuna wakati inabdi tuamini katika matokeo. Matokeo sio lazima yaambatane na uwezo. Kuna timu zinapata matokeo ambayo hayaendani na uwezo wake. Binafsi Messi anawapa sabuni waargentine lakin wao wanampaka matope. He might do something leo ili angalau mashabiki wake wapate cha kuongea, sio lazima afunge lakini timu ipate matokeo.

Wasiposhinda leo wajiandae kutafuta nauli ya kurudi kwao.

By Privaldinho na Aziz.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here