Home World Cup URUSINI: Ronaldo kutoa hukumu kwa timu nyingine ya Afrika

URUSINI: Ronaldo kutoa hukumu kwa timu nyingine ya Afrika

9907
0
SHARE

Leo Jumatano, fainali za kombe la dunia zinaendelea kutakuwa na mchezo wa Kwanza wa kundi B mchezo huo utachezwa mida ya saa tisa kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki. Mchezo huo utakuwa kati ya Portugal, dhidi ya Morocco, utapigwa katika dimba la Luzhiniki Stadium.

Taarifa kwa timu zote mbili.

Portugal, leo atashuka dimbani kutafuta ushindi baada ya mchezo wao wa Kwanza dhidi ya Hispania, kutoa sare ya mabao 3-3. huku nyota wao Cristiano Ronaldo , alifunga hatrick yake ya 51 katika maisha yake ya soka.

Portugal, wanaamini kuwa safu yao ya ulinzi itacheza vizuri tofauti na mchezo wao wa Kwanza waliruhusu mabao matatu. Katika safu hiyo ya ulinzi leo itaongozwa na Bruno Alves, na Jose Fonte, huku beki wao Jorge Santos, akiwa bado majeruhi.

Kocha wa Portugal, Fernando Santos, amesema kuwa anafurahi kuona kiwango cha nyota wake Cristiano Ronaldo, akicheza juu ya kiwango.

“Tunaenda kucheza na Morocco, naamini Ronaldo, atacheza mechi yake kubwa na tumejipanga vizuri kwenye mchezo wetu wa leo,”.

“Portugal, walikuwa Mabingwa wa Ulaya, kwa sababu Ronaldo, alikuwa nahodha wa kikosi wa timu hiyo,”.

Morocco, mchezo wao wa Kwanza walipoteza dhidi ya Iran, walipoteza kwa bao 1-0.mchezo wetu dhidi ya Mabingwa wa Ulaya utakuwa mchezo wetu mgumu.

Morocco, watawakosa mabeki wao wawili Nordin Amrabat, na Nabil Dirar, ambao wapo majeruhi.

Kocha wa Morocco, Herve Renard, amesema kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Portugal, itakuwa ngumu mno kumzuia Ronaldo, hata kama tukitaji sare tunahitaji mikakati ya kumzuia Ronaldo.

“hata kama tukimueke Ronaldo, akabwe na watu watatu na wachezaji wengine wa Portugal, watakabwa na nani.

“Portugal, wana washambuliaji wengi ambao wanaweza kucheza vuzuri na wao ni Mabingwa wa Ulaya,”.

Tukumbuke.

Mara ya mwisho Morocco, walicheza na Portugal, fainali za kombe la dunia ilikuwa Mwaka 1986 nchini Mexico.

Vikosi vinavoweza kuanza leo.

Portugal.Patricio, Ledric, Pepe, B. Alves, Guerrero, William, Mountinho, B. Silva, Mario, Andre Silva, Cristiano Ronaldo.

Morocco. El Kajoui, Hakimi, Saiss, Benatia, Mendyl, El Ahmadi, Ziyach, Boussoufc, Belhanda, Amrabat, Boutaib.

by Admila Patrick

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here