Home World Cup RUS2018: Diego kwenye mtego wa deni la Ronaldo

RUS2018: Diego kwenye mtego wa deni la Ronaldo

9042
0
SHARE

Kutakuwa na mchezo wa kundi B Katika fainali za kombe la dunia mchezo huo utachezeka majira ya saa tatu kamili usiku kwa saa za Afika Mashariki. Spain, atacheza na Iran, katika dimba la Kazan Arena.

Iran, watamkosa beki wao wa kati Rouzbeh Cheishmi, atakosa fainali hizo baada ya kusumbuliwa na maumivu ya misuli aliumia mazoezini.Khanzadesh ,anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo katika safu ya ulinzi ya Iran. Iran, mchezo wao wa Kwanza walibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Morocco.

Kocha wa timu ya taifa Iran, Carlos Quieroz, amesema kuwa wamejiandaa vizuri na mechi yetu dhidi ya Spain. tumepata nafasi ya kucheza na timu bora duniani.

“kama yataweza kutokea majabu katika mchezo wa soka basi tutaweza kuwazuia Spania,”.

“tunatakiwa kucheza katika ubora wa hali ya juu na mwisho wa siku matokeo yataamua,”.

Spania, watanza mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya mchezo wao Kwanza kutoa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Portugal. Watu wengi wakimpinga kiwango cha Degea, lakini Fernando Hierro, jana alisema Degea, atacheza mchezo wao dhidi ya Iran. huku akisema mshambuliaji wake Diego Costa, ataiongoza safu ya ushambuliaji. Huku akisema Daniel Carvajal, amepona majeraha yake ya nyama za paja na ataweza kuanza mchezo wa leo kuchukua nafasi ya Nacho.

Kocha wa Spain, Fernando Hierro, amesema kuwa Daniel Carvajal, amefanya mazoezi na timu na ameonyesha kiwango kizuri.

Ronaldo leo ameongeza bao la 4. Diego Costa ana deni la mabao mawili kumfikia Ronaldo leo usiku

“Degea, leo anacheza na matumaini moja ya makipa bora duniani,”.

Tukumbuke.

Iran, haijawahi kushinda katika michezo 6 , aliyokutana na timu za Ulaya. Amepoteza 5, sare 1 , kushinda 0.

Vikosi vinavoweza kuanza.

Iran. Beiranvand, Rezaien, Poualiganji, Khanzadeh, Hassafi, Johanbaksh, Shojaei, Ebrahimi, Amiri, Ansarifard, Azmoun.

Spain. Degea, Carvajal, Pique, Ramors, Alba, Bosquet, Koke, Iniesta, Silva, Costa, Isco.

By Aziz Mtambo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here