Home Kimataifa Rekodi usizozijua zilizowekwa Urusi hii leo

Rekodi usizozijua zilizowekwa Urusi hii leo

12818
0
SHARE

Ureno 1 – Morocco 0, Bao pekee la Cristiano Ronaldo dhidi ya Morocco linamfanya kufikisha mabao 85 ya kimataifa, idadi hii inamfanya Cristiano kuwa mchezaji wa Ulaya mwenye mabao mengi zaidi ya mechi za kimataifa.

Bao hili hili la Cristiano Ronaldo linamfanya kuwa mchezaji wa pili baada Jose Torres (1966) kuwa mchezaji wa pili kuwahi kufunga mabao kwa mguu wa kushoto, mguu wa kulia na kichwa katika mashindano ya kombe la dunia.

Uruguay 1 – Saudi Arabia 0,  kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la dunia, timu ya taifa ya Uruguay imefanikiwa kishinda michezo miwili ya mwanzo katika kombe la dunia.

Mchezo wa leo ulikuwa wa 100 kwa Luis Suarez kwenye timu ya taifa, na goli alilofunga Suarez linamfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Uruguay kufunga bao katika michuano 3 mfululizo, alifunga 2010, akafunga 2014 na mwaka huu.

Katika michuano yote ya mwaka 2014 kulikuwa na ushindi wa bao 1-0 mara 8 katika hatua ya makundi, lakini mchezo wa leo wa Uruguay na Morocco umeifikia rekodi nzima ya makundi mwaka 2014 kwani mechi ya leo ni ya 8 kwa timu kupata ushindi wa 1-0 msimu huu.

Spain 1 – Iran 0, tarehe 25 mwezi June mwaka 1982, tarehe 23 June 2010 ndio siku mbili pekee ambazo kulikuwa na mechi 3 ambazo timu zilishinda 1-0, ushindi wa leo wa Hispania umeiingiza siku ya leo katika siku hizo.

Hadi hivi sasa hakuna mechi hata moja katika kombe la dunia ambayo imeisha kwa sare ya 0-0, mara ya mwisho kwa kombe la dunia kuchezwa mechi nyingi bila sare ya 0-0 ilikuwa 1954 ambapo zilipigwa mechi 54 bila sare kama hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here