Home Ndondo Cup Perez adai mchezo unaokuja ni fainali

Perez adai mchezo unaokuja ni fainali

9297
0
SHARE

Achana na makelele ya Misri na Morocco kutemwa katika michuano ya kombe la dunia. Leo tupo ubungo maeneo ya kinesi. Vijana wa Tandika walipambana vyema na vijana wa Stimu tosha. Mchezo ulikuwa wa kasi sana hasa kipindi cha kwanza ambapo timu zote zilitoka sare ya bila kufungana. Mchezo ulikuwa mgumu hasa baada ya kuona kadi mbili zikitoka kwa upande wa Tandika.Kevini Kiduku kiungo huyu hatari kabisa aliongoza jeshi la Stim Tosha kujaribu kufuta fedheha ya kichapo cha mchezo wa awali kutoka kwa UV Tmk.Timu zote zimeingia kwenye mpambano huu zikiwa zimefungwa jumla ya mabao 7.

Mchezo wa kwanza Stim tosha walianza na mabeki Ibrahim Job na Dickson Chota kama mabeki wa kati. Mfuko alitumika kama kiungo wa kati lakini mchezo ule alizidiwa kwa kiasi kikubwa na viungo wa UV TMK. Mchezo wa leo Mfuko amerudishwa kama beki wa katika na kusimama imara.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Tandika walionekana kuelemewa zaidi. Stim Tosha walipata nafasi kadhaa baada ya madhambi kufanyika katika eneo lao la hatari. Kevin kiduku alishindwa kabisa kuvusha mipira yote miwili ya adhabu katika ukuta wa wapinzani wake.

Baada ya makosa kadhaa Kelvin Kiduku alitumia nafasi murua baada ya kupokea krosi akatulia na kuweka mpira kambani.mchezo ulikamilika kwa Stimu tosha kuibuka na Ushindi. Kocha mkuu wa Stim Tosha Bwana Adam Perez alisema anawasifu wachezaji wake kwa upambanaji. Amekiri timu kukosa washambuliaji mbadala. “Tuna changamoto ya washambuliaji. Timu inamtegemea Kevin Sabatho Peke yake. Hilo kwetu halitukatishi tama. Mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Kauzu tutacheza kama fainali. Ni kweli kauzu wana mashabiki wengi lakini sisi hatuogopi hilo.Kocha mkuu wa Tandika amesema timu yake haikuwa na bahati. “Sina wa kumlaumu, wachezaji wangu wamejituma kwa moyo wote. Bahati haikuwa kwetu”Alipoongelea mchezo wao wa mwisho dhidi ya UV Tmk alisema “Huo mchezo tutakwenda kushindana licha

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here