Home Kitaifa Pamoja na upofu, lakini shabiki huyu anaamini furaha yake iko kwenye Ndondo...

Pamoja na upofu, lakini shabiki huyu anaamini furaha yake iko kwenye Ndondo Cup

9444
0
SHARE

Ni siku nyingine niko kwenye viwanja vya Ndondo Cup kuangalia kandanda safi la watoto wa kitaa, na hii leo nilikuwa uwanja wa Bandari Tandika kwa mchezo kati ya Kauzu Fc vs Uv Temeke.

Mchezo unamalizika kwa suluhu ya bila kufungana lakini wakati mechi ikiendelea nilivutiwa sana na mashabiki wa Kauzu, kama kawaida yao wakiongozwa na Chief walikuwa wakipiga kidedea kila mara.

Safari hii nimevutiwa na bwana mmoja mnene aliyekuwa anaimba sana, wakati namsogelea nilishangaa kugundua bwana huyu hakuwa anaona(alikuwa kipofu), nikashtuka na kupata shauku kuzungumza naye.

Anasema yeye haoni kabisa, hakuzaliwa na tatizo hili lakini mwaka 1999 ndipo alilipata baada ya kufanyiwa upasuaji na kuanzia hapo hakuwa tena na uwezo wa kuona na ndio sababu hata uwanjani hapo anatembea kwa kushikwa mkono.

Anadai kwamba furaha yake na kitu kinachomvutia kwa sasa ni Ndondo Cup, na anajisikia faraja kuwa mshabiki wa Kauzu Fc, japokuwa haoni ila vibe waliyonayo inamfanya kupata faraja ya moyo. Nimekuwekea You Tube video ya maongezi ya mimi na shabiki huyu wa Kauzu Fc

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here