Home Kitaifa Manula matumaini kibao tuzo za VPL 2018

Manula matumaini kibao tuzo za VPL 2018

8520
0
SHARE

Baada ya kamati ya tuzo ya mchezaji bora Tanzania bara kwa msimu uliomalizika kutangaza orodha ya wachezaji katika vipengele mbalimbali wanaowania tuzo hizo, golikipa wa Simba Aishi Manula anaamini anastahili kushinda tuzo ya kipengele cha kipa bora.

Tuzo hizo zinazoandaliwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF) zinatarajiwa kufanyika June 23, 2018 Dar es Salaam.

“Kwangu ni kitu kikubwa na kizuri, kwa magolikipa tunaoshindania tuzo hiyo ni wazuri na tumeweza kufanya vizuri kwenye vilabu vyetu ndiyo maana tumebaki watatu katika kipengele hicho”-Aishi Manula.

“Ukizungumzia kilichotokea kwenye ligi msimu huu, najiona nina sababu za kushinda tuzo hiyo ukiangalia ‘clean sheets’ zangu kwenye mechi za ligi nilizocheza, timu yangu imeweza kushinda ubingwa kwa hiyo nina matumaini katika hilo.”

Endapo Manula atashinda tuzo ya golikipa bora VPL 2017/18  itakuwa ni tuzo yake ya tatu mfululizo, hadi sasa ameshashida tuzo hiyo mara mbili mfululizo lakini mara zote alikuwa golikipa wa Azam FC.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here