Home Kimataifa MTAZAMO: Shaffih Dauda kuhusu timu za Afrika kuanza vibaya kombe la dunia...

MTAZAMO: Shaffih Dauda kuhusu timu za Afrika kuanza vibaya kombe la dunia 2018

9584
0
SHARE

Afrika tunawakilishwa na timu tano kwenye fainali za kombe la dunia, mataifa matatu tayari yamepoteza mechi zao za kwanza huku Misri yenyewe ikipoteza mechi mbili za kwanza hatua ya makundi.

Senegal ndiyo lilikuwa tumaini la mwisho kwa waafrika na kweli wamelibeba bara la Afrika baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Poland, Shaffih Dauda ametoa mtazamo wake kwa nini mataifa mengine yameshindwa kupata matokeo lakini Senegal wameanza vizuri kwa kupata pointi tatu.

Wakati mwingine pia inachangiwa na mpangilio wa makundi hii ina maanisha unacheza na nani. Timu zote za Afrika ambazo zimetangulia kucheza mechi na kupoteza angalia watu waliocheza nao.

Misri ilikutana na Uruguay miongoni mwa timu ambazo zina uwezo mkubwa sana unapozungumzia fainali za kombe la dunia. Nigeria ilifungwa na Croatia ambayo ni moja ya timu bora kwa sasa Ulaya kutokana na aina ya wachezaji iliyokuwa nao.

Tangu Croatia ilipofuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza na mwaka 1998 wanakuwa washindi wa tatu Ufaransa hawajawahi kushindwa kufuzu tena kwenye fainali za kombe la dunia.

Morocco ilipoteza mchezo wake dhidi ya Iran ambao walikuwa wanafanana viwango hata ukiangalia mechi na namna ambavyo Morocco walifungwa ni mechi ambayo ililingana ushindani.

Timu nyingine ya Afrika kupoteza mchezo ilikuwa Tunisia ambayo ilifungwa na England.

Miongoni mwa timu zote za Afrika Senegal ndio timu ambayo ipo kwenye kundi ambalo linaweza kutoa ushawishi huenda Senegal ikafuzu kutokana na aina ya timu za kundi hilo (Poland, Colombia na Japan).

Katika mchakato wa kufuzu kutoka bara la Ulaya, Poland walifuzu wakiwa vinara wa Kundi lao ambalo nafasi ya pili ilishikwa na Denmark lakini ni kundi ambalo zilikuwepo timu kama Montenegro, Romania, Armenia, Kazakhstan kwa hiyo siyo kundi ambalo lilikuwa gumu kwa Poland.

Senegal kutokana na maandalizi waliyofanya na kucheza kama timu kukawapa matokeo tofauti na timu nyingine kutoka Afrika ambazo zilikuwa zinapambana na timu zenye ushindani mkubwa.

Kitu kingine naweza kusema bahati pia ilikuwa upande wa Senegal, goli la kwanza ambalo Poland walijifunga liliwapa faida baadae kipindi cha pili M’baye Niang akafunga bao la pili na wenyewe wakaruhusu goli dakika za mwisho ambao kama umefatilia vizuri utakuwa umegundua timu za Afrika zimeruhusu magoli dakika za mwisho kabisa kwa hiyo hata Senegal wasingekuwa wametangulia kufunga mapema tungekuwa tunasimulia story nyingine.

Senegal wana nafasi nzuri kwa sababu timu yao imekaa pamoja kwa muda mrefu na wana malengo ya kupata mafanikio kwa hiyo mimi nawapa nafasi kama wawakilishi wa Afrika ambao watasogea mbali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here