Home Kimataifa Kunani kila mtu Brazil? Hadi Kyombo na Manula nao wapo Brazil!!

Kunani kila mtu Brazil? Hadi Kyombo na Manula nao wapo Brazil!!

9270
0
SHARE

Timu ya taifa ya Brazil ndiyo inatajwa kuwa ina mashabiki wengi zaidi duniani katika michuano ya kombe la dunia na katika mashindano ya mwaka huu (2018) ndiyo timu inayopewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo licha ya kuanza kwa sare.

Ukiachana na Juma Kaseja, Mrisho Ngasa, Joti, Nikki II, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva na wengine wengi mashambuliaji Habibu Kyombo na golikipa Aishi Manula nao ni miongoni mwa watanzania wanaoishabikia Brazil.

Kyombo amesema amekuwa shabiki wa Brazil kwa sababu baba yake alikuwa anainga mkono kitambo sana tangu yeye akiwa mtoto.

“Timu ninayoishabikia ni Brazil na ndio timu ambayo ninaipa nafasi ya kuchukua ubingwa kwa sababu inawachezaji wengi vijana halafu wanatamani kupata mafanikiomakubwa hapo lazima utamzungumzia Neymar ambaye ana ndoto ya kuwa mchezaji bora wa dunia.”

“Naipenda Brazil kwa sababu inaamini vijana halafu nikijikuta naipenda tangu mdogo maana ndiyo tumu ambayo baba alikuwa anaishabikia.”

“Neymar anapojituma kwa ajili yakushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ndio anavyoisaidia timu, halafu wachezaji wengi wa Brazil wana vipaji hiyo ndiyo sababu inanifanya niwape nafasi kubwa.”

Akiwa mchezaji kuna vitu anavyojifunza kupitia  kombe la dunia au anaangalia burudani tu?

“Kwanza lazima tukubali wenzetu wametuzidi kwa hiyo unapoangalia mashindano haya unajifunza vitu vingi, kila mechi unayoangalia unakutana na vitu vigeni kwa hiyo najifunza mambo mengi kutoka kwao.”

“Mimi ni striker kwa hiyo huwa naangalia kile ambacho kinafanywa na strikers ili niwe bora.”

Role model wa Kyombo katika mashindano ya mwaka huu ni Cristiano Ronaldo kwa sababu jitihada zake na kujituma kwake ndiyo kumemfikisha hapo alipo na anafanya watu wengi waamini kila kitu kinawezekana.

Ukija kwa Tanzania One Aishi Manula na yeye yupo hukohuko kwa wabrazil, anasema alianza kuvutiwa na Brazil ile ya akina Ronaldo de Lima, Dida, Carlos, Rivaldo na wengine.

“Timu yangu ninayoishabikia mwanzo mwisho ni Brazil kwa sababu tangu nikiwa mdogo watu wakizungumzia timu za taifa utasikia Brazil tukienda kwenye vibanda umiza watu wengi wanazungumzia Brazil enzi hizo ya kina Ronaldo de Lema wakati mimi ndio nilikuwa nakua.”

Kama ilivyo kwa Kyombo, kuna magolikipa ambao Manula anawafuatilia na kuchukua ujuzi kwao ili umsaidie katika kuboresha uwezo wake.

“Kwa upande wa Brazil tunamwangalia zaidi Neymar lakini pia wapo Ronaldo na Messi lakini katika nafasi ya golikipa ambayo nacheza mimi  wapo wengi De Gea, Coutoius na wengine wengi ambao nitakuwa nawaangalia ili kujifunza kupitia wao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here