Home Kitaifa Habibu Kyombo asiyependa bata alivyoamua kuichagua Singida na kuitosa Simba

Habibu Kyombo asiyependa bata alivyoamua kuichagua Singida na kuitosa Simba

8955
0
SHARE

Zoezi la usajili linazidi kupamba moto huku vilabu vya Simba, Singida United na Azam vikionekana kufanya usajili mapema tofauti na timu nyingine.

Mshambuliaji aliyesajiliwa na Singida United hivi karibuni Habib Kyombo amevunja ukimya nakuzungumza baada ya usajili wake.

“Kwangu naamini Singida itakuwa klabu na wachezaji nitakaokutana nao tutafanyakitu kizuri kuweza kuisaidia timu kupata matokeo na mataji.”

Kuna tetesi zilimhusiah Kyombo kutakiwa na Simba na Azam lakini mwisho wa siku akasaini Singida, mwenyewe anasema muda bado wa kwenda Simba, Yanga na Azam.

“Ukisema timu kubwa hata Singida nayo piani timu kubwa, halafu ni timu ambayo naweza kupata muda mwingi wa kucheza. Haimaanishi ningeenda sehemu nyingine nindeshindwa kucheza ila Simba na Yanga timu kubwa na kila mtu anatamani kwangu mimi naona muda bado, ukifika nitacheza.”

Kyombo ameingia fainali (wachezaji watatu wa mwisho) kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa VPL, hatua hii imemuongezea chochote?

“Imeniongezea vitu vingi, kwanza kujituma zaidi kwa sababu kuwa miongoni mwa hao si kazi ndogo unatakiwa kujituma ili msimu ujao nipate zaidi ya hiki.”

Anapambana na Shabani Idd Chilunda (Azam) Yahya Zayd (Azam) lakini Kyombo anaamini yeye ni bora na anastahili kushinda tuzo hiyo.

“Ni wachezaji wazuri, wana kila sifa kakini mimi pia ni mchezaji mzuri nadhani nastahili kushinda hiyo tuzo kwa sababu nimefanya vizuri.”

Hafagilii ‘bata’ bata kabisa

“Nashinda home naangalia movies, nacheza game, jioni naenda mazoezi kidogo siku yangu inakuwa imeisha hivyo huwa sitoki.”

“Kupumzika pia ni bata kwa hiyo inategemea tu mwenyewe, naamini ukipumzika ni zaidi ya bata kwa hiyo kwangu kupumzika ni bora zaidi.”

Kama hujui, Kyombo kabla ya kujiunga na Mbao amepita kwenyentimu nyingi. Alianzia BQ Academy ampo alilelewa kwa miaka nane halafu akajiunga na Simba B ambapo hakukaa sana akasajiliwa na Lipuli akacheza mzunguko wa kwanza mzunguko wa pili akaenda zake Mbao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here