Home World Cup URUSINI: Ushindi wa Senegal na ushirikina wa Afrika

URUSINI: Ushindi wa Senegal na ushirikina wa Afrika

15803
0
SHARE

Senegal wametisha sana. Senegal wamevunja rekodi ya Poland ya kutoka kufungwa na timu yoyote ya Afrika. Ni bao la kujifunga la mapemaThiago kunako dakika ya 37. Hii ni kwa mara ya pili Senegal wanapata bado dakika ya 37. Mwaka 2002 Camara kwenye mchezo dhidi ya Sweden alifunga bao dakika ya 37. Baadae Niang alitumia mwanya wa makosa ya mpira uliopigwa kimakosa, maarufu kama boko na kuweka kambani bao la pili kunako dakika ya 60. Krychowiak aliwapatia wapolish bao la kusawazisha dakika ya 86.

Hakika wanahitaji pongezi. Michezo minne dhidi ya timu za ulaya haijafungwa mchezo wowote alama 8, suluhu michezo miwili, na kushinda miwili. wamechez michezo 6 ya kombe la dunia wamepoteza mchezo mmoja tu katika hatua ya robo fainali dhidi ya Uturuki bao la Ilhal dakika ya 94. Wamefunga mabao 9 na kuruhusu 7 pekee.

Hii ni mara yao ya pili katika kombe la dunia. Mwaka 2002 walikwenda fainali hizi wakiwa na mchezaji mmoja tu ambaye anacheza ligi ya ndani ajulikane kama Khaliodou Cissokho ambaye alitokea ligi ya Afrika akitokea Horoya ya Guinea. Zamu hii haina mchezaji hata mmoja kutoka bara la afrika.

Kwanza kidogo niwatolee uvivu au povu.

Watu wengi huwa tunapenda sana kujiona wajuaji. Sijui ni asili yetu au ni kujionesha kwamba nasi tunaweza kutoa hoja. Nilikuwa nasubiri Senegal wanipe sababu hasa kwanini niongee.

Tumekuwa wanafiki sana kwa timu za Afrika. Na huu unafiki wetu ndio ushirikina wetu mkubwa unaotutafuna sisi wenyewe. Sisi sio wavumilivu na hatupendi kuishi katika uhalisia. Yaani tunakwenda kununua Range Rover lakini mfukoni tuna hela ya Vitz. Watu wanazilaumu timu za Afrika kufanya vibaya. Naona kama tunazibebesha lawama ambazo zinazidi uwezo wao. Kwanza muundo wa mashindano ya Afrika hauwezi kwenda sawa na kasi ligi mbalimbali. Usishangae kuona baadhi ya mataifa ya Afrika kufanya vibaya ikiwa tunafahamu wazi sababu ni zipi.

Leo hii Msiri anashindana na ushelisheli, sijui Cape Verde unategemea watapata vipi ushindani wa kutosha kupambana na timu za Afrika na Amerika. Huu ni ushirikina mkubwa mno kuamini kwamba timu zetu zinafanya vibaya kwa makusudi au viwango vibovu.

Ugumu wa soka letu unahitaji wetu asilia wa soka hili hili. Ni ngumu sana msukuma kuwafundisha kijaluo wahehe. Tunahitaji mtu anaykwenda sawia na uhalisia au ladha halisi ya soka letu. Juzi niliandika kwamba ushirikina mkunwa tulio nao ni kuamini kwamba makocha wa kizungu watainua soka letu.Tangu lini injinia wa maghorofa akajenga nyumba ya Makuti?

Kuamini kwamba tunahitaji akina Cuper na Herve Renhard kutupeleka hatua ya 16 bora huo ni ushirikina.

Aliou Cisse alikuwepo kwenye kikosi cha 2002 kilichotolewa na Uturuki. Leo hii ameiongoza Senegal kutoa dozi kwa Wapolishi. Kwanini hata Simba na Yanga zisiwaamini akina Matola. Matola na wenzake akina Kiemba wao ndio wanaojua ladha yetu haswa. Hawa akina Lanchrate ni akina Cuper wengine walioshindwa kumtumia Salah ana elneny vizuri.

Kwanza mimi naona timu za Afrika zimejitahidi kwa kiasi kikubwa potelea mbali matokeo mabovu ya Morocco dhidi ya Iran, pamoja na uzembe wa Misri wao wenyewe katika mchezo wao dhidi ya Urusi.

Tunisia imepambana na timu ambayo ligi yao ni bora dunia hadi dakika ya 92. Misri wamehakikisha Mshambuliaji bora wa Hispania Suarez na Mshambuliaji bora wa Ufaransa Cavan wasifunge. Je kwa jitihada hizi bado mnawapuuzia? Hapana sisi tuwanafiki.

Kosa sio timu zilizofuzu kosa ni uchumi wa bara la Afrika. Umasikini ndio tatizo kubwa kwenye ukuaji wa soka letu la Afrika. Wala sio vipaji. Kinachokuzungusha kinadumuza au kukulemaza au kukukuza. Soka letu la Afrika lipoje? Ushindani wake unaleta chachu ya sisi kupambana?

Mpaka sasa tumefungwa mabao 10 na tumeshinda matano katika michezo sita ya awali.

Ni mchezo mmoja tu timu ya Afrika imeruhusu zaidi ya mabao mawili. Kiuhalisia timu za Afrika zimepambana kwa kiasi kikubwa. Angalieni timu bora kama Ujerumani zinafungwa na wauza unga wa Mexico, angalieni Brazil ilivyoteseka kwa watoto walaini wa Uswisi? Angalieni Messi alivyoshindwa kuifunga timu ambayo ndio kombe lao la kwanza la dunia??

Angalieni hao wachimba chumvi ywa Panama yalivyofungwa mabao mengi kama kikapu? Tuna kila sababu ya kukubaliana na aina ya matokeo tunayopata. Hii ni sawa na tumebeti jero tupate milioni 500. Misri wametoka nje utupu kwa sababu umeme umekatika kwa bahati mbaya umeme umerudi wakiwa bado hawajarudi ndani. Kichapo cha Misri leo kilikuwa sahihi kabisa.

Wameenda uwanjani kupambana kiume. Wamejitoa kwa hali na mali. Leo hakwenda kuzuia. Walikwenda kutafuta matokeo. Unapokwenda vitani unaenda na matokeo mawili kufa au kupona.

usisahau kunifollow Instagram kwa jina la Privaldinho (na usiahau kuingia dauda tv youtube)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here