Home Kimataifa URUSINI: Taarifa kuhusu majeraha ya Neymar

URUSINI: Taarifa kuhusu majeraha ya Neymar

10853
0
SHARE

Mchezaji tegemezi wa Brazil Neymar amepata majeraha mazoezi hivi leo akiwa na timu yake ya taifa wakiajiandaa na mzunguko wa raundi ya pili katika hatua ya makundi ya kombe la dunia.

Kocha mkuu wa Brazil Titte alimpa siku moja ya mapumziko Neymar lakini leo alionekana akiondoka mazoezini akiwa anachechemea. Walikuwa wakijiandaa na mtanange wa pili dhidi ya Costa Rica.

Neymar ameumia enka ya mguu wa kushoto katika mpambano wao dhid ya Switzerland na sio mguu uliovunjika.

Daktari Rodrigo Lasmar amesem Neymar aliondoka kwa tahadhari baada ya kujisikia vibaya. Neymar anatarajia kufanya vipimo zakdi ili kugundua tatizo hasa lina ukubwa gani.

Kwenye mchezo dhidi ya Switzerland alifanyiwa madhambi mara 10 rekoddi kubwa zaidi kwenye kipindi cha miaka 20 iliyopita kwenye mashindano ya kombe la dunia.

Coutinho amesema kwamba, Uswisi walicheza mpira wa kukamia zaidi huku wakicheza kwa dhamira ya kuyaka kuwaumiza wachezaj wa Brazil.

Pia amesema hali ya Neymar ipo sawa na anaendelea vyema

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here