Home Kimataifa URUSINI: Macho yote kwa Salah leo

URUSINI: Macho yote kwa Salah leo

7619
0
SHARE

Kuelekea mechi ya leo jumanne,ya group A kati wenyeji Russia dhidi ya Egypt, katika uwanja wa Krestovsky. Hizi ni taarifa za timu

Russia: Wenyeji watakuwepo bila Alan Zzagoev, ambaye alitokea benchi katika mechi dhidi ya Saudi Arabia. Alikuwa anasumbuliwa na majeraha,na anaonekana anaweza kukosa mechi zote zilizobaki. Inaonekana nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Denis Cheryshev ambaye alitokea benchi na kufunga mabao mawili katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Saudi Arabia.Mlinzi Yuri Zhirkov alifanya mazoezi peke yake jumapili, kutokana na kupata tatzo la kifundo cha mguu.Hivyo anaoneka kuwa fiti katika mechi ya leo jumanne.

Egypt: Macho ya watu wengi yatakuwa kwa kikosi cha Egypt kitakachoanza, na wengi tunasubiri taarifa za Salah kama yuko fiti kuanza au laah.Mshambuliaji huyo ambaye yuko kiwango kizuri hakuwepo kwenye mechi dhidi ya Uruguay. Japokuwa anaonekana kuwa fiti,na Egypt wamepoteza mechi ya kwanza, Mafarao hao wanatakiwa kumuanzisha mchezaji huyo muhimu, kama watataka kupiga hatua kwenye group lao. Salah ataangaliwa kama yuko fiti kabla ya mechi. Ila itastaajabisha sana kama mchezaji huyo wa Liverpool hatacheza.

Mitazamo ya makocha wa timu zote mbili katika mkutano na waandishi wa habari.

Kocha wa Urusi Stanslav Cherchesov ameweka wazi kuwa,timu zinatakiwa zikimbie haraka na kutumia mbinu zozote bila kujali timu inayochezanayo. Na timu yangu sio ya kipekee.Nina imani na timu yangu, nina imani na wachezaji wangu na tuko tayari kufanya hili na tutafanya.

Kocha Egypt Hector Cuper amesema, kujiandaa na mchezo wenyewe unahusisha mjadala kuhusu Salah, lakin Cuper ameweka wazi kuwa, Egypt sio timu ya mtu mmoja.
Kila kocha ana mbinu zake, na wanajiandaa kwajili ya mechi kulingana na falsafa yao wenyewe.Alisema, ” Mo Salah ni mchezaji mmoja, nafikiri itakuwa vyema zaid kama Russia watamfikiria yeye.

Ni mchezaji muhimu ,mchezaji wa kushangaza,lakini sijaandaa timu imtegemee mchezaji mmoja.

Kumbukumbu
Timu hizi hazijakutana kabla,Russia haijafungwa na timu za Afrika katika kombe la dunia yangu mwisho wa muungano wa Soviet.Egypt haikuruhusu goli katika kombe la dunia mwaka 1990.

Vikosi vinavyotegemewa kuanza

Russia: Aknfeev, Zhrikov, Ignashevich, Kutepov,Fernandez, Gazinaski, Zobnin, Sheryshev, Golovin, Samedov, Zyzuba

Egypt: Elshanawy, Abdel-shafy, Hegazy, Ali Gabr, Fathi, Elneny, Hamed, Trezeguet, Abdalla, Warda, Salah.

Makala na Admila Patrick

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here