Home World Cup URUSINI: Jeshi la Falcao vitani dhidi ya Samurai

URUSINI: Jeshi la Falcao vitani dhidi ya Samurai

7665
0
SHARE

Leo Jumanne, kuelekea fainali za kombe la dunia saa tisa kamili mchana kutakuwa na mchezo wa kundi H kati ya Colombia, dhidi ya Japan, mchezo huo utapigwa katika dimba la Mordovia Arena.

Taarifa za timu.

Colombia, kuelekea fainali za kombe la dunia Mwaka 2014, waliishia robo fainali walitolewa na Brazil, kwa jumla ya mabao 2-1.

Nyota wa Colombia, James Rodriguez, pia aliibuka mfungaji bora wa Mwaka 2014, kule nchini Brazil, huenda leo asianze mchezo wa leo baada ya kupata majeraha ya misuli akiwemo na kiungo wao Wilmar Barriors.

Kocha wa Colombia, Jose Peckerman, akisema kuwa vitu hasaivi vimebadilika tumebadili wachezaji tuna timu bora nafikiri timu yetu bora na ina nguvu.

Japan, walipoteza michezo miwili ya kirafiki walipoteza dhidi ya Ghana, na Switzerland.

Kocha wa Japana, Akira Nishino, toka amechukua timu hiyo Mwezi wa nne ameiongoza michezo mitatu tu.

Japan, wachezaji wao wawili ambao walikuwa majeruhi amerudi kikosini ambao Shinji Kagawa, na Keisuke Honda, huku kiungo wao anayechezea Leicester City, Shinji Okazaki, bado anaumwa maumivu ya nyonga.

Kumbukumbu.

Colombia, mara ya mwisho walimfunga Japana, mabao 4-1 katika fainali za kombe la dunia za Mwaka 2014, huku nyota wa Colombia, James Rodriguez, akifunga mabao mawili.

Vikosi vinavoweza kuanza Leo.

Colombia. Ospina, Arias, Mina, D. Sanchez, Mojica, Uribe, Aguilar, C. Sanchez, Cuadrado, Bacca, Falcao.

Japan. Kawashima, Endo, Yoshinda, Nagatoma, Sakai, Shibasaki, Yamaguchi, Muto, Kagawa, Inui, Osako.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here