Home World Cup Matukio ya Kombe la Dunia- Russia jana

Matukio ya Kombe la Dunia- Russia jana

7942
0
SHARE

Melkizedeck Mbisse

1- Kieran Trippier, mchezaji wa Uingereza jana katika mchezo dhidi ya Tunisia aliweka rekodi katika timu ya Taifa la Uingereza “Three Lions” kutengeneza nafasi 6 za magoli na kuwa mchezaji wa pili toka mwaka 1966 kutengeneza idadi kubwa baada ya David Beckham kutengeneza nafasi 7 katika mechi dhidi ya Trinidad na Tobago mwaka 2006.

2. Harry Kane baada ya kufunga magoli 2 dhidi ya Tunisia, ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kuwafunga makipa wawili katika mechi moja katika michuano ya kombe la Dunia, baada ya Diego Forlan kufanya hivyo dhidi ya Afrika Kusini mwaka 2010.

3. Harry Kane amefikisha magoli 150 tangu kuanza kwa msimu wa 2014/15, magoli 15 katika hayo yakiwa yakiwa dhidi ya timu ya Taifa na 135 yakiwa dhidi ga klabu yake ya Tottenham Spurs.

4. Romelu Lukaku baada ya kufunga magoli 2 dhidi ya Panama jana anakua amefikisha magoli 15 katika mechi 10 za mwisho kwa timu yake ya Ubeligiji/Belgium. Ni mchezaji wa kutazamwa katika michuano hii pia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here