Home World Cup URUSINI: Waingereza na mapovu yao itakuwaje?

URUSINI: Waingereza na mapovu yao itakuwaje?

10535
0
SHARE

Maswali mengi yameulizwa mitandaoni sana, achilia mbali magoli matatu ya Ronaldo, wala Penati ya Messi au Machozi ya chicharito. Wala siongelei nywele za Neymar nazungumzia Kikosi cha England na filamu ya Love Island. Kuna wadau wengi kule England washaanza mdomo. Toleo jipya la hii filamu ya Love Island linaendelea. Wapo wanaosema bora waendelee na filamu yao kuliko kumuangalia Rashford na Jones wanacheza.

Mitandao inaathiri kwa kiasi kikubwa kuharibu viwango vya wachezaji maana waimgereza wengi hawana subira wala uvumilivu.

Rio anasema
“Wachezaji wengi watakata tamaa kutokana na komenti za mashabiki. Hizo komenti wazipotezee kwanza. Watulie hasa hasa mambo yanapokwenda mrama. Wakae kwa kutulia wala hata wasihangaike kuzisoma maana zina udhi”

England leo watakutana na wawakilishi wa Afrika Tunisia. England wanpaswa kucheza kwa tadhahri kubwa katika mpambano huu jasa baada ha matokeo ya awali ya timu kubwa kama Brazil na Ujerumani.

England watapambana na Tunisia katika kiwanja cha Volgograd muda wa saa 3 usiku.

Kumekuwa na ubishani mkubwa katika upangaji wa kikosi cha England.

Rashford aanze’

“Kwangu mimi Marcus Rashford Anapaswa kuanza na sio Raheem Sterling,” amesema mshabiki mmoja kutoka England alipohojiwa na jarida la Bbc ajukikane kama Adam.

“Anacheza kwa kasi sana, anajituma na ana uchu wa kufanikiwa, binafsi huyu ni mchezaji anayepaswa kuvaa jezi ya timu ninayoipenda”

Dier

“hili ni swali gumu sana kwangu kwamba nani aanze kati ya hawa jamaa Jordan Henderson au Eric Dier,” swali hili aliulizwa Daniel.

“kwakweli sioni kama Dier ana nafasi kwenye kikosi cha Gareth Southgate lazima atawekwa benchi tu.

Cahill
Mshabiki mwingine Joshua Lowe amesema Cahil hapaswi kuanza.

“Itabidi waanze Kyle Walker, John Stones na Harry Maguire huyo Gary Cahill simwamini sana.

Takwimu
Akili za Waingereza bado zinawaza ubingwa wao wa mwaka 1966. Watunisia wao wanawaza rekodi yao ya timu ya kwanza kutoka afrika na timu ya kwanza ya kiarabu kupata ushindi kombe la dunia.

England wanatumia zaidi mfumo wa 3 5 2 ambao umeifanya kuwa na ulinzi imara zaidi. Wameruhusu mabao 11 tu katika michezo 18, ikiwa wameruhusu mabao matatu pekee kwenye michezo 10 ya mwisho. Lakini licha ya kuwa mshambuliaji mzuri (Hary Kane) anayefananishwa na Alan Shearer ambaye aliongoza England mwaka 1998 wakicheza na Tunisia bado hawafungi mabao mengi. Wamefunga mabo 10 tu kwenye michezo 9. Ushindi wao mnono wa mwisho ulikuwa dhidi ya Malta mabao 4 kwa bila mwezi wa 9 mwaka jana.

Tunisia sio imara sana lakini wameruhusu mabao 6 tu kwenye michezo 8 ya kufuzu. na kuruhusu mabao matano tu kwenye michezo ya 6 ya mwisho. Mchezo wao na Ureno walionesha ukomavu wa hali ya juu kwa kutoka nyuma kwa mabao mawili na kutoka sare bila kusahau mechi yao dhidi ya Uhispania ambapo walifungwa bao moja tu.

Mchezo wa mwisho wa England dhidi ya timu za afrika walitoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Algeria kule Afrika kusini 2010. Kama unakumbuka vyema mchezo ule mashabiki wa England walimzomea Wayne Rooney. Hii ndio sababu kubwa ya Rio kuwasihi wachezaji kupotezea mitandao kabisa.

Mwisho ni hili. Mchezaji bora wa England, mwenye rekodi nzuri ya mabao kwa dakika, mwenye magoli mengi kuliko wote, ambaye kwa sasa anakipiga klabu ya London ya kaskazini na Si Mwingine ni Danny Welbeck!!

Nawaombeni wote mumkaribishe huyu kijana kwa moyo wote.

Unaweza ukauliza Danny Welbeck??? Ndio Danny Welbeck the Billy Bill blanks Chakraboti Mr Pank. Ana mabao 16 licha ya ufinyu wa nafasi. Je Welbeck aanze au asieanze?? kikosi cha England wewe unakionaje? watatoka kwa waarabu?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here