Home World Cup URUSINI: Shida sio rangi ya Lukaku, ila No Harry in Afrika

URUSINI: Shida sio rangi ya Lukaku, ila No Harry in Afrika

9472
0
SHARE

Michezo ya leo imekamilika tayari. England wametoka na Ushindi wa Mabao mawili kwa Moja dhidi ya Tunisia mabao mawili ya Harry Kane pamoja na bao pekee ya Tunisia likifungwa na Sassi kwa njia ya tuta. Mapema kabisa Sweden walipata ushindi kiduchu wa bao 1 dhidi ga Korea kusini bao pekee la Granqvist kwa mkwaju wa penati. Ubelgiji walitoa dozi nene kwa Panama. Mabao mawili kutoka kwa mshambuliaji hatari Romelu Lukaku akifunga mawili huku Mertens wa Napoli akifunga moja.

Hakuna sababu ya kuwa na makocha wa kizungu. Tunisia wamefungwa sawa, lakini angalau wameonesha uhai. Ni tofauti kidogo na wana misiitu wa Nigeria waliokwenda ulaya kwenye maonesho ya mavazi ya linda mazingira yakutunze ya jezi zao. Tunisia wamepambana sana. Chini ya mwalimu wao mzawa Nabil ambaye amechezea taifa hilo michezo 74. Wana utofauti kabisa na Wamisiri chini ya Cuper au Morocco chini ya Herve.

Mwisho wa siku lazima tukubaliane kombe la dunia limekuwa gumu sana mwaka huu kama ilivyo roho na Sura ya Raisi wa Urusi. Mechi zilizochezwa ni 14, mabao yaliyofungwa dakika za mwisho mwisho kuanzia dakika ya 89 ni 6 kati ya mabao 32 yalikwisha fungwa. Ni michezo mitatu tu iliyoweza kuzaa mabao zaidi ya matatu.

Harry Kane akiwa na kitambaa mkono wake wa kushoto amefanya kile alichoshindwa kukifanya Wayne Rooney kule Afrika kusini dhidi ya Algeria.

Akiwa kama nahodha amefanya tukio ambalo sisi wataalamu tunaliita No Harry in Afrika.

Kwanini nasema no Harry in Afrika? Afrika katika michezo minne imeruhusu mabao sita na kufunga 1 tu. Maana yake Harry Kane ana mabao mengi kuliko washambuliaji wote wa Afrika.

Kwanza Harry Kane ameonesha mshambuliaji unapaswa kuwa eneo gani na kwa wakati gani na ufanye tukio gani.

Afrika hatuna washambuliaji wabunifu. Hatujui tufanye nini na kwa wakati gani. Timu zinacheza na presha kubwa na kutokujiamini. Watu wanadhani labda kuzaliwa Afrika au kuwa mwafrika ndio tatizo! hapana sio kweli. Mbona hawa hawa akina Iwob wanafanya vyema huko ulaya? Shida iko wapi?

Shida ni baadhi ya washambuliaji wetu hawafanani na washambuliaji kama akina Kane kiuchezaji. Lukaku ni mchezaji mweusi kama hawa hawa wa Afrika tatizo ni moja tu apotoka huko kwa wazungu tukija tunakosa makocha wenye falsafa zinazokidhi matakwa ya soka letu halisi. Mwisho wa siku timu inaingia uwanjani kuzuia tu.

Wachezaji ni wale wale lakini Je tunawatumia vipi. Ndio Maana ukiangalia mpira wa Tunisia wamecheza kwa kuelewana vizuri kwa sababu kuna mwalimu ambaye analijua haswa soka la taifa lake na wachezaji wake wanahitaji nini

Magoli yote ya Kane hajatumia nguvu wala hajalazimisha mabeki wakamkabe ila ametulia kana kwamba hayupo uwanjani lakini ana malengo yake binafsi. Lukaku amefunga mabao mawili kwenye mchezo wao wa awali mapema hivi leo je sio mweusi kama sisi?

Tukiachilia mbali matokeo hayo. Tunisia wamefanya vyema. Ukiachilia mbali ugumu wa kundi lao unaweza kusema kama wangepangwa kwenye kundi jepesi kama la Misri au la Morocco wazungu wangewakoma. Kwa bahati mbaya sana Tunisia mchezo ujao wanakwenda kukutana na Lukaku. Hii ni bahati mbaya sana kwao. Nafadhaika sana kuona Tunisia wanaondoshwa mapema

Nimeangalia mechi za ufunguzi. Timu za Afrika zote zimeanza michezo migumu sana. Yaani ukiangalia kwa mbali labda Morocco ambao nao hawajielewi kwa kufungwa na watengeneza vinu vya nyuklia huko Iran. Sijajua hasa mechi za Afrika kwanini zote ni ngumu au ni namna ya kuzipunguza kasi mapema kabisa ama vipi.

Watalaamu wa mambo wanasema tunahitaji robo fainali yenye kuvutia na sio ya ngekewa. Hali bado ni ngumu mno kwa timu za ukanda wa Afrika. Karata ya mwisho ni kwa Senegal yenye wachezaji nyota kama Sadio Mane, Sakho, N.k

La mwisho usiahau kufuatilia Dauda Tv youtube pia usisahau kunifollow Instagram kwa jina la Privaldinho na kupata habari murua kwenye akaunti ya shaffih instagram

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here