Home World Cup URUSINI: Xhaka mdomoni mwa timu inayopendwa zaidi duniani

URUSINI: Xhaka mdomoni mwa timu inayopendwa zaidi duniani

12887
0
SHARE

Mabingwa hawa mara tano wa kombe la dunia watacheza mchezo wa kwanza wa kiwa na rekodi ya kutokufungwa mchezo wa ufunguzi tokea 1994 dhidi ya Italy.

Kipute hiki kitatia nanga katika uga wa Rostov Arena muda wa saa 3 usiku.

Brazil watatupa karata yao dhidi ya Switzerland ikiwa chini ya kamanda Granit Xhaka. Uswis wana rekodi yao kubwa ya kuwa timu pekee iliyowahi kuwafunga mabingwa katika mchezo wa ufunguzi kule afrika kusini mwaka 2010 walipokutana na Hispania.

Wabrazil wanarudi tena katika fainali hizi baada ya kupata kipigo che fedheha kayika ardhi yao mwaka 2014.

wakiwa chini ya kocha Tite Brazili walijitwalia tiketi ya kwenda Urusi ikiwa kaama timu ya kwanza kabisa kutoka bara la amerika kusini.

Ni wachezaji 6 tu wenye uzoefu na kombe la dunia katika kikosi cha wazee hawa samba wenye soka lenye ladha ya kila namna.

Juma Kaseja anasema yeye anaishabikia Brazil kwakuwa inaonekana kuwa ndiyo timu inayopendwa zaidi. Kuna uwezekano mkubwa kweli kwamba Brazil ndiyo timu inayopendwa zadi. Mzee Akilimali mwenyewe anakwambia tokea akiwa mtotto yeye alikuwa ni Brazil. Kisoka yeye ni Mbrazil huku sababu kubwa kwake ni kwa sababu wanavaa njano kama Yanga.

Brazil wataenda kukutana na timu ambayo imefungwa mchezo mmoja tu tokea mwaka 2016 bila kusahau maajabu waloyofanya katika michuano ya Yuro walipotolewa kwa mikwaju ya penati.

Uchambuzi wa wachambuzi mahiri

Giancarlo Giampietro, kwa Upande wa Brazil
Nina imani kubwa kwamba A Seleção wanapaswa kucheza kwa uvumilivu na umakini mkubwa kwa sabab Uswissi wao watacheza kwa tahadhari kubwa na kwa kujizuia zaidi. Waswisi wanaweza kucheza mpira wa kuboa kwa nguvu na kasi kubwa ya ukabaji ambayo kwa namna moja ama nyingine kama wabrazil wasipokuwa makini wanaweza kupaniki na kukosa lengo. Kuna uwezekano mkubwa Tite akawaanzissha Neymar, Gabriel Jesus, Philippe Coutinho na Willian, kwa lengo la kujaza zaidi ubunifu mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji na kuwahada walinzi kwa ufundi wao.

Alan Schweingruber, Upande wa Switzerland

Kwa heshima zote tunatambua uwezo wa wabrazil lakini hatuna hofu yoyote kwani bado tuna harufu ile ya kutoka suluhu dhidi ya Hispania na ushindi mnono dhidi ya Japan katika mechi za kujiandaa. Kocha wetu mkuu Vladimir Petkovic najua tayari ameshapata mbinu mbadala za namnaa ya kupambana na presha ya wabrazili. Uswis watakumbuka ushindi kiduchu waliopata Argentina dhidi yao kule Brazil 2014 hivyo wakitaka kufanikiwa zaidi wanapaswa kuongeza juhudi na kujitoa wanaweza kuibuka na alama.

PATAKA KIFURUSHI

Brazil wameshinda michezo 16 ya ufunguzi kati ya 20 kwemye kombe la dunia. Wamepoteza michezo miwili kipindi kile wakiwa bado wanavaa jezi nyeupe.ck in the days when they played in white. Mchezo wa kwanza walifunga 2-1 na Yugoslavia kule nchini Uruguay mwaka 1930 kisha wakapokea kicchapo cha mbwa koko cha mabao 3-1 kutoka kwa Spain katika fainali zilizofanyika Italy mwaka 1934.

Utabiri wa Vikosi

Brazil: Alisson; Danilo, Thiago Silva, Miranda, Marcelo; Casemiro, Paulinho, Philippe Coutinho; Willian, Gabriel Jesus, Neymar.

Switzerland: Sommer; Lichtsteiner, Schaer, Akanji, Rodriguez; Behrami, Xhaka; Shaqiri, Dzemaili, Zuber; Seferovic.

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu Gabriel Jesus Vs Firmino nani atumike zaidi kama namba 9. Upi mtazamo wako nani aanze katika nafasi hiyo.

By Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here