Home World Cup URUSINI: Timu za Afrika tunayumba wapi

URUSINI: Timu za Afrika tunayumba wapi

9410
0
SHARE

Hali si nzuri kwa timu za Afrika kombe la dunia..

Na Elizabeth Lyavule

Tuliingia mashindanoni tukiwa na matumaini makubwa kwa timu zetu za Afrika lakini mambo yamekua tofauti kwani katika michezo ya ufunguzi, timu tatu kati ya tano zimepoteza mechi zao nakuzua sintofahamu kama watavuka katika makundi kwenda hatua inayofuata ya 16 bora au watafungasha virago mapema kuyaaga mashindano.

kwasasa wamebaki Senegal na Tunisia kutuaminisha walau wanaweza sogea mahali maana kwakucheki kila kundi alilopo muafrika ni wazi ndoto za kuvuka kwenda hatua ya 16 bora zinafifia.

Nigeria yupo kundi gumu sana kundi la kifo, akiwa kashapoteza mchezo wake wa ufunguzi kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya taifa la Croatia anashika mkia katika msimamo wa kundi na mechi ijayo anakutana na Argentina mwenye njaa ya pointi tatu kujiwekea hai matumaini ya kufuzu je ataweza pata matokeo?pia kuna timu kama Iceland si ya kubeza ni timu nzuri ndiomana wamegawana pointi na Argentina kwa sare ya goli 1-1, haitakua ajabu Nigeria akimaliza wa mwisho katika kundi tofauti na matarajio ya wengi waliompa nafasi ya kusonga mbele.

Misri amepoteza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya Uruguay dakika chache kabla mpira kumalizika kwakukubali kufungwa goli 1-0 , ingawa walicheza vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa bado walifeli kufunga magoli hivyo wamejiwekea mlima wa kupanda ili wafuzu 16 bora kwani kundi lake kuna timu mwenyeji Urusi na kibonde Saudi Arabia kama atashindwa kupata alama tatu dhidi ya mwenyeji asahau kuvuka. Huenda ujio wa Mohhamed Salah kwa ajili ya mechi ijayo ukaongeza makali katika safu ya ushambuliaji na kutibu tatizo la kuchezea nafasi wanazozipata

Morroco naye kama ndugu yake Misri alikubali kupoteza mchezo katika dakika za nyongeza kipindi cha pili dhidi ya Irani nae akafungwa 1-0, katika kundi lake yupo na timu ngumu kama Hispania na Ureno ni wazi kaweka rehani mashindano haya, uhakika wa kuvuka kwake ni mdogo sana kutokana na uzito wa kundi alilopo

Macho na matumaini yetu waafrika ni kwa timu zilizobaki Senegal na Tunisia kama nao watafanya vibaya michezo yao ya ufunguzi tutabaki kuwa vichwa vya mwendawazimu kama kawaida yetu rangi nyeusi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here