Home World Cup URUSINI: Neymar anayumba, Wajerumani watusamehe kitambaa hakikutoshi

URUSINI: Neymar anayumba, Wajerumani watusamehe kitambaa hakikutoshi

17598
0
SHARE
Kilichotokea leo sio tu kimeishangaza dunia pia hata kuzimu huenda bado mjadala unaendelea. Mabingwa wakubwa wa dunia ya soka wanasimamishwa mchana kweupe. Sio Brazil sio Ujerumani.

Ujerumani wamefungwa bao moja kwa bila kutoka kwa Mexico, bao pekee kutoka kwa Lozano.

Wajerumani walihitaji hata sare lakini kwa bahati mbaya kitamabaa hakikutosha.

Brazil wametoka sare ya bao kwa moja na Switzerland. Mabao ya Phillipe Coutinho na Zuber kwa upande wa Uswisi. Mpambano huu ulikuwa kati ya Uswis matajri ambapo ndipo benki kuu ya dunia ilipo, na Wabrazil ambao wengi wametokea maisha magumu hasa hadithi ya Gabriel Jesus ambaye 2014 alikuwa mpaka rangi huko kwao Sao Paolo. Kuna watu wachokozi sana. Kuna jamaa amenitumia meseji akaniambia tatizo la Brazil hawajui kuwa jezi wanayovaa ina gundu sana msimu huu.

Mambo niliyojifunza leo

Kwa wajerumani tunaweza tukaamini kwamba kuna wakati huwa mambo yanakataa. Abdi Banda aliwahi kuniambia kuna siku mnaweza kwenda uwanjani kila kitu kikawa hakiendi sawa hata kidogo. Ni kweli nikaukumbuka mpambano kati ya Arsenal na CSKA Moscow ambapo Thiery Henry alitamani ardhi ipasuke azame chini. Leo Ujerumani hatuwezi kusema kwamba Walimkosa Leroy Sane au Bastian au hata Ballack. Mambo yaligoma tu. Sio kwamba Mexico walitawala sana kwa kumiliki mpira la hasha ni sehemu ya soka.

Jambo la Pili
Ndio kuna uwezekano wa mipango mibovu ya mwalimu hasa goli la kwanza na baadhi ya magoli waliokosa Miexico kwa uzembe wao. Kma wangekuwa na umakini mkubwa basi wangeshinda magoli zaidi ya moja. Mwalimu Jog Low alijiamini sana kama alivyojiamini kwenye uchaguaji wa kikosi chake. Goli walilofungwa walifungwa kwa mfumo wao waliouzoea wao kuwaadhibu wenzao, yaani kaunta ataki. Alijimiamini sana kwa kucheza mpira wa ofensivu zaidi yaani kushambulia sana kuliko kujilinda. Tulimuona Toni, Khedira wakicheza dimba la juu, Mats alipanda mpaka katikati kati ya uwanja. Mfumo huu uliwapa nafasi kubwa ya wa Mexico kukimbia bila bughudha kwani asilimia kubwa ya viungo walikwenda kushambulia.

Jambo la tatu

Hili nimeliona kwa Wabrazil. Hivi majuzi niliwaambia marafiki zangu kwamba Hazard ana umuhimu mkubwa kwenye timu kuliko Neymar. Hazard anacheza kitimu. Anaangalia kwanza timu inahitaji nini. Baadhi waliona kama naamdharau Neymar lakini kwa maono yangu mchawi mkubwa wa Brazil ni Neymar. Kikosi cha Brazil ni kizuri mno. Kila mchezaji ana uwezo binafsi. Hakuna mwenye kipaji cha kuungaunga kama Giroud na Welbrck, labda tu Augusto Renato ambaye bado ni mzuri kuliko hata Henderson.
Neymar hachezi kitimu anacheza kiubinafsi.

Hili ni kombe la dunia, asidhani kana kwamba anacheza na Rennes ya kule ufaransa. Ningekuwa mwalimu Titte, Neymar angekwenda Benchi ningeendelea na shughuli na Douglas Costa.

Jambo la nne
Wachezaji wa Brazili na Wabrazil kwa ujumla, wanaishi kwa mazoea. Wamekremisha maisha.

Kipindi cha kwanza walikuwa wanacheza ovyo ovyo. Lengo lao ni kujaribu kucheza samba. Wanajisahau kwamba samba haiwezekani hasa ukitazama kwamba asilimia kubwa ya wachezaji wake wanacheza ulaya katika ligi tofauti tofauti ambazo asilimia kubwa hawaabudu samba. Zamani Wabrazil walicheza Brazil na wengine walijificha Italia. Sasa hivi hadi china wapo, Sio china tu hata Singida United wapo.
Wamejijengea kwamba Jesus lazima awe kama De lima.

Na wanaabudu hiyo jezi namba 9. Yule Jesus wa kazi gani kule uwanjani? Huyu kipindi cha De lima asingepewa hata ruhusa ya kubeba maji kwenye timu au angepigwa marufuku kununua jezi ya De lima. Yaani mchezaji mdogo kama Jesus akabidhiwe jukumu la wa brazili takribani milion 300? Noo No No. Ana kipajo sawa. Kikubwa tu, lakini ni mchanga sana. Wanatudanganya. Jesus hajakaa kimajukumu. Hajakomaa kiupambanaji bado ni kijana mduchu sana. Kila mmoja amemuona. Firmino aanze tu. Hakuna namna

Jambo la nne
Nimejiuliza sana ile video ya marefarii kwani imeletwa kwa ajili ya wazungu tu au pia na mataifa mengine? Samahani lakini. Juzi Argentine yalitokea matuta mawili ya wazi lakini mwamuzi wala hakujisumbua. Nimeshangaa sana ile faulo nyepesi ya Griezmann VAR imeona lakini leo Zuber kumsukuma Miranda wala sio tatizo. Yule Jesus naye alikumbatiwa na hata kama alijirusha kwa kuchelewa lakini bado faulo ilichezwa je mwamuzi alisimamisha mchezo? VAR ni usumbufu tu kwa hili wamefeli.

Jambo la tano
Neymar anataka Ballon d’Or ipi kwani? Hii hii ya Messi na Ronaldo au Sallom d’or? Kama ni Sallon d’Or bila shaka kwa utengenezaji wa nywele wake sina kipingamizi. Nimeona kichwa ameweka sijajua ni tambi spesho au zile za pakti.

Enewei, Neymar anapaswa kufanya kitu kimoja. Asiwe na mazoea na mpira kabisa. Ajifunze kupitia Ronaldo sio Messi. Ni rahisi sana kujifunza kupita Ronaldo na ukafanikiwa kuliko Messi. Messi ana kitu cha ziada ambacho ni yeye tu anacho kwa kuzaliwa ila sio kwa kujifunza au mazoezi, Labda na wewe uzaliwe nacho (Kujiamini kusiko kwa kawaia na wepesi wa maamuzi katika mazingira yenye uwekano duni). Ronaldo ana jitihada, kipaji na mjanja kitu ambacho ukikipambania unaweza kufanikiwa ingawa sio lazima ufanikiwe kama yeye. Ronaldo akikaa sana na mpira hana madhara makubwa kuliko akiwa hana mpira. Messi akikaa na mpira ni mbaya zaidi na njia rahisi kumdhibiti ni kumzunguka wanne kama walivyofanya Iceland.

Neymar mchezo wa leo alikuwa akikaa na mpira muda mwingi huku akizubaisha mashambulizi. Bibi yangu aliniambia ukichezea kinyesi kinaweza kukurukia usoni. Neymar anachezea sana kinyesi mwisho wa siku kimewarukia usoni. Hafanyi maamuzi kwa haraka na hii itaikwisha timu kiujumla

Jambo la Mwisho
Usisahau kunifollow Instagram kwenye account yangu ya Privaldinho. Pia usichoke kufuatilia Dauda Tv youtube upate uhonda wa soka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here