Home Kimataifa Ujerumani vs Mexico, Low anaanza kuifukuzia rekodi ya Vitorrio Pozzo

Ujerumani vs Mexico, Low anaanza kuifukuzia rekodi ya Vitorrio Pozzo

10021
0
SHARE

Baada ya mitanange kadhaa hatimaye leo moto unaendelea kuwaka pale nchini Urusi, kwa mara ya kwanza mabingwa watetezi wa michuano hiyo, timu ya taifa Ujerumani wataanza safari ya kulitetea kombe lao dhidi ya Mexico.

Juan Carlos Osorio kocha wa timu ya taifa ya Mexico anakuja katika mchezo huu akiwa na kumbukumbu mbovu dhidi ya Ujerumani ambapo mwaka jana tu alikubali kipigo cha bao 4-1 toka kwa timu B ya Ujerumani.

Mwaka 1985 timu hizi za taifa ziliwahi kukutana katika mchezo wa kirafiki na ndio mechi pekee ambayo Mexico waliwahi kuifunga Ujerumani, lakini katika michezo 10 iliyobaki baina yao wakasuluhu 5 na kufungwa 5.

Kombe la dunia mwaka huu ni muhimu sana kwa kocha wa Ujerumani Joachim Low kwani anatafuta rekodi ya kocha wa timu ya taifa Italia mwaka 1934 Vittorio Pozzo ya kushinda kombe la dunia mara mbili mfululizo.

Katika michuano ya kombe la dunia hii sio mara ya kwanza kwa timu hizi mbili kukutana na mara yao ya kwanza ilikuwa 1978 katika hatua kama hii ambapo Mexico walikufa kwa mabao 6-0.

Imepita miaka 40 sasa tangu mara ya mwisho kwa timu ya taifa ya Ujerumani kushindwa kufunga katika mechi yao ya mwanzo ya ufunguzi wa kombe la dunia, mara ya mwisho ilikuwa 1970 wakati wa mechi dhidi ya Poland.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here