Home Kitaifa “Mpira una gharama, ni mzigo kwa kiwanda”-Mkurugenzi Mtibwa Sugar

“Mpira una gharama, ni mzigo kwa kiwanda”-Mkurugenzi Mtibwa Sugar

9834
0
SHARE

Kwa taarifa yako, kiwanda cha kuzalisha sukari Mtibwa hakipati faida kutoka kwa timu yake ya Mtibwa Sugar badala yake kiwanda ndio kinatumia mkwanja mrefu kwa ajili ya kuendesha timu.

Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Jamal Baisa amezungumza na Mkazuzu na kuthibitisha kwamba kiwanda bado kinasaidia uendeshaji wa timu hiyo katika masuala ya fedha.

“Kwa sasa hivi kiwanda ndio kinachangia kwa kiasi kikubwa pesa za uendeshaji wa timu licha kwamba tunapata kiasi cha pesa kutoka Azam na Vodacom, tuko mbioni kutafuta wadhamini ili tushirikiane nao kuiendesha timu kwa sababu mpira una gharama kubwa na ni mzigo mkubwa kwa miwanda.”

“Viwanda vingi vikubwa TBL, Sigara, vimeachana na mpira, una gharama kubwa na hauleti faida ya moja kwa moja. Mfano sisi Mtibwa hatuuzi sukari nyingi zaidi ya Kilombero kwa sababu tuna timu ya mpira.”

“Timu inasaidia kwa kiasi fulani lakini lengo ni kuwapa burudani wafanyakazi wa Mtibwa na kujenga michezo nchini kusaidiana na serikali kuboresha michezo ili kupata vijana wa kuimarisha timu ya taifa lakini si kwamba kuna faida nyingine ambayo kampuni inapata kupitia mpira.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here