Home Dauda TV Mbwiga akaacha kutangaza ‘live’ kavamia kigoma cha Ndondo

Mbwiga akaacha kutangaza ‘live’ kavamia kigoma cha Ndondo

10040
0
SHARE

Uzalendo ulimshinda mtoto wa Kizaramo Mbwiga Mbwiguke ‘mzee wa mkole wa nyani kibwaya mkia’ hiyo ni baada ya kujumuika kwenye shangwe la mashabiki wa Banda waliokuwa wakisherekea ushindi wao wa magoli 3-1 dhidi ya Ubungo Terminal.

Mashabiki wa Banda walikiwasha kigoma chao kwa mwanzo mwisho lakini kilipamba moto baada ya timu yao kupata bao la tatu na hapo Mbwiga akaona ubaya-ubaya tu watakaosema yeye ni shabiki wa Banda na waseme lakini haachi kwenda kukisakata kigoma.

Akasahau kazi iliyompeleka uwanjani ya kutangaza mechi hiyo live badala yake akaanza kuyarudi akiwa na mic yake mkononi, kweli Ndondo noma jamani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here