Home Kitaifa Coastal Union yasajili beki wa Zanzibar Heroes

Coastal Union yasajili beki wa Zanzibar Heroes

9895
0
SHARE
Adeyum Ahmed Saleh (kulia) wakati akiitumikia Zanzibar Heroes kwenye mashindano ya Challenge Cup 2018

Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ wameanza kujenga kikosi chao kwa ajili ya msimu mpya wa VPL 2018/19  kwa kusajili beki wa pembeni wa Kagera Sugar na timu ya taifa ya Zanzibar Adeyum Ahmed Saleh na kiungo Yakubu Kibiga kutoka Majimaji FC ya Songea.

“Mpaka sasa tumesajili wachezaji wawili, mmoja ni mchezaji wetu alizoeleka hapa alikuwepo wakati timu inashuka daraja Adeyum ambaye alikuwa anacheza Kagera lakini amemaliza mkataba wake na mchezaji mwingine ni Yakubu Kibiga alikuwa Majimaji, wote tumewapa mikataba ya mwaka mmoja”-Stephen Mguto, Kaimu Mwenyekiti Coastal Union.

“Kuna wachezaji 10 ambao tunataka kuwasajili kuungana na wachezaji wengi 15 ambao wamebaki baada ya timu kupanda ligi kuu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here