Home Kitaifa Yanga, Azam, Singida zangongana kusajili Mtibwa

Yanga, Azam, Singida zangongana kusajili Mtibwa

12168
0
SHARE

Yanga, Singida United na Azam zimegongana katika harakati za kutaka kumsajili golikipa wa Mtibwa Sugar Benedict Tinoco ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar.

Tinoco amesema bado mazungumzo yanaendelea kati ya timu hizo na uongozi wa timu yake kwakuwa bado ana mkataba kwa hiyo kama mchezaji anaheshimu mkataba wake.

“Bado nina mkataba wa mwaka mmoja ndaniyaMtibwa Sugar hicho ndio kinanipa ugumu hadi sasa sijajua hatma yangu kuelekea kwenye vilabu hivyo.”

“Suala la kutafutwa na vilabu hivyo lipo lakini shida inakuja kwamba mimi bado nina mkataba na timu yangu ya Mtibwa ndio maana hakuna hakuna mazungumzo yoyote kwa sababu bado nipo chini ya watu.”

“Mkataba inabidi uheshimiwe, sina uamuzi wowote kwa sababu mimi si mchezaji huru nasubiri mazungumzo yao kama yataenda vizuri mimi nipo tayari kucheza popote kwa sababu mpira ndio kazi yangu.”

“Bado sijaambiwa mazungumzo yamefikia hatua gani kwa sababu ni mapema sana, naendelea kusubiri kila kitu kikiwa sawa wataniambia wameamua nini.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here