Home World Cup URUSINI: Tuliyoyaona kwa Messi na wenzake

URUSINI: Tuliyoyaona kwa Messi na wenzake

12148
0
SHARE

Argentina kuna shida gani tena? Wazungu wanasema Iceland ni Surprise Package. Yaan tunaita kibubu cha kushtukiza. Kitu kisichotarajiwa. Iceland wameishangaza dunia. Wamejitahiddi kuhahakikisha wamemdhibiti vyema Lionel Messi.

Messi amekosa penati ya 25 katika historia ya maisha yake. Penati tatu zaidi ya mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo. Penati hii ingefufua upya matumaini ya Argentina.

Hatuwezi kusema Messi amekosea wapi. Ni uongo mtakatifu tukianza kukaa chini na kuanza kujadili Messi alipaswa kufanya nini. Sampaolo ndiye wa kulaumiwa zaidi. Mezza kuanza mbele ya Dybala ni kioja. Kuna kila sababu mwalimu Sampaolo akawa mchawi wa taifa lao.

Messi amejituma kuhakikisha anawafurahisha mashabiki wake. Bahati haikuwa kwake. Ni siku ngumu sana katika maisha yake hasa ukiangalia amekosa mkwaju wa penati.

Mambo matano ya muhimu

Jambo la kwanza
Tatizo lingine ni sehemu ya kiungo wa kati. Ever Banega bila shaka anapaswa kuanzakila mchezo ili kuongeza kasi na chachu katika eneo hilo. Mascherano sip mbunifu kiasi kile.

Jambo la Pili
Argentine bado inamhitaji sana Romero. Mlinda mlango wa Man United Sergio Romero aliachwa kwenye kikosi baada ya kuumia goti. Willy Caballero ambaye hajawahi kucheza mchezo wowote wa mashindano na jezi ya taifa lake alipewa nafasi hiyo leo. Leo ameigharimh timu yake baada ya kushindwa kuokoa krosi mbili nyepesi kabla ya shuti la tatu kulipangua vibaya na kumkuta Alfreo Fannboguson. Sampaolo anapaswa kufanya uamuzi kwa makipa wake wawili Guzman na Franco.

Jambo la tatu
Sirggurdson na Aron wametawala sana dimba hasa kwa kaunta ataki (Mashambulizi ya kushtukiza). Sirgudson ameweza kukamilisha mikimbio minne mbele ya Biglio na Mascherano.

Jambo la nne.
Safu ya Ulinzi ya Iceland ni chuma cha reli. 2016 Ronaldo alipiga mashuti 10 na hakufunga kabisa. Messi amepiga mashuti 11 na hajafunga. Hii ni alama mbaya kabisa kwa wapinzani wengine. Mashuti 7 yamezuiliwa au kublokiwa kwa maana nyingine. Bila shaka wapo vizuri. Hivyo Messi amekutana na mawe.

Jambo la tano

Shida kubwa kwa Argentina inaonekana kuna ubutu kwenye suala la bahati. Yaani bahati imekuwa finyu kwao. Wanategeneza nafasi nyingi lakini hazizai matunda. Mchezo wa leo Iceland wamelizingira lango lao na kuhakikisha hakuna shuti litakalopenya.

Jambo la Mwisho
VAR ni mchezo wa kumfunga paka kengele. Dakika ya 77 Pavon aliangushwa dhahiri eneo la hatari. Mwamuzi hata hakwenda kuomba msaada wa marefarii wa nje. Tusemeje sasa? Vipi yule beki kunawa mpira eneo la hatari? Je Otamend kushika mpira? Hapana kwakweli. Akina Collina wanapaswa kujitathmini upya. enewei hata hizo penati Messi angepewa bado angekosa (Natania tu)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here