Home Kimataifa URUSINI: taarifa za Croatia Vs Nigeria

URUSINI: taarifa za Croatia Vs Nigeria

8065
0
SHARE

Leo jumamosi tunaangalia tena mchezo wa kundi D kati ya Croatia V Nigeria, mchezo ambao utachezwa majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za afrika mashariki.

Taarifa kutoka timu zote

Kwa upande wa Croatia, hawana majeruhi na wanategemea kutaja mastaa wote wakiwemo Luca modric,Ivan Rakitic,Vedran Corluka na Mario Mandzukic.

Mshambuliaji wa Croatia Nikola Kalinic amesema, Kitu muhimu sasa ni pointi zote tatu.Tuna ubora kwenye kushambulia, hatuwezi kuogopa, kitu cha muhimu ni kwamba, tunacheza vizuri na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wetu.

Nigeria: Mlinzi wa Nigeria, Leon Balogun, anaweza kukosa mechi baada ya kukosa mazoezi yaliyofanyika Alhamis, na Kenneth Omeruo anasubiri mchezaji Wilfred Ndidi ili aweze kuchukua nafasi yake, pamoja na kwamba alikuwa ana majeraha,Odion Ighalo anaweza kuiongoza safu ya ushambuliaji, akishirikiana na Khelechi Ihenacho.

Kocha wa Nigeria Gemot Rohr anasema, Timu tunayo kwa muda mrefu, tulikuwa nayo pia kwenye mechi za kufuzu, Nina uhakika tutawafanya Wanaigeria wafurahi.Tuna team ya vijana wadogo, labda hili kombe la dunia ni la mapema mno kwao.Tuna kikosi cha wachezaji wadogo, hivyo 2022 ndo litakuwa kombe lao la dunia.Tunataka kuwafanya watu wa Nigeria wafurah lakin sio matokeo tu, ni tabia na jinsi tunavyocheza mpira, unaweza kuleta thaman kwa hii nchi kubwa.

Croatia na Nigeria ndo mara ya kwanza kukutana, na Croatia wana rekodi mzuri kwa team za Afrika.

Vikosi vinavyotarajia kuanza

Croatia: Subasic,Vida,Corluka,Lovren,Strinic, Badejil,Rakitic,Modric,Rabec,Mandzukic,Perisic

Nigeria
Ozoho,Omeruo,Troots- Ekong,Ogushehu,Iwobi,Mikel,Ndidi,Idowu,Mozes, Ighalo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here