Home World Cup URUSINI: Hakuna uchawi wa kumzuia Messi

URUSINI: Hakuna uchawi wa kumzuia Messi

7843
0
SHARE

Iceland itakuwa taifa dogo kabisa katika fainali za kombe la dunia watakapokutana na Argentina in Moscow.

Kiungo wa Iceland Gylfi Sigurdsson anatarajia kurejea uwa jani baada ya kuumia goti wiki iliuopita walipokuwa wakiumana na Ghana

Mkufunzi wa Argentina Jorge Sampaoli aliwashangaza wengi baada ya kutaja kikosi chake siku moja kabla.

Argentina XI: Willy Caballero, Eduardo Salvio, Nicolas Otamendi, Marcos Rojo, Nicolas Tagliafico, Lucas Biglia, Javier Mascherano, Maximiliano Meza, Lionel Messi, Angel di Maria, Sergio Aguero.

Tathimini

Licha ya kupata mafanikio makubwa katika ardhi ya wageni (Barcelona) lakini bado Messi ana deni kubwa sana ndani ya taifa lake. Kule Brazil licha ya kufika fainali dhidi ya Ujerumani Messi alirudi muflisi nyumbani.

Messi ni kama amebingita biwi la moto kuhakikisha anajibu mapigo ua Cristiano Ronaldo ambaye jana ametandika hat trick yake dhidi ya Hispania.

Akiwa na miaka 31 je ana kombe lingine la dunia lijalo kweli? binafsi itakuwa natia chuku nikisema kama atakuwa kwenye kiwango hiki miaka minne ijayo.

Kikosi chao kimekumbwa na lawama nyingi baada ya Mauro Icardi kuachwa huku Leo Messi akisemekana kuhusika.

Kwanza wiki iliyopita Messi alipoulizwa kuhusu kustaafu timu ya taifa alisema itategemea na hatua tutakayofika.

Hali ya Messi sio mamati sio hayati kwenye hatma ya timu yake ya taifa.

Messi amefunga magoli 7 kati ya 19 kwenye hatua ya kufuzu bila kusahau hat trick iliyowapeleeka kombe la dunia.

Asilimia 90 ya Albiceleste ni Messi kurudia maajabu ya Maradona ya mwaka 1986. Mchezo wa dhidi ya Hispania bila ya Messi walikula kipigo cha mbwa kula pilau ya eid cha mabao 6-1.

Rekodi kubwa ya Iceland ni kile kipigo cha Euro 2016 dhidi ya England katika hatua ya robo fainali.

Kocha mkuu wa Iceland Heimir Hallgrimsson amesema mpambano huu ni kihistoria katika taifa lao. Alipoulizwa kuhusu Messi :”kuhusu Messi, kwakweli sijui nitumie uchawi gani, Maana kila mtu amejaribu kumzuia na bado amekuwa akifunga hivyo sijui nitatumia muujiza gani”

“Yule ni mchezaji bora wa dunia anajua kila kitu na ana uwezo mkubwa sana. Haguwezi kusema tutamkaba yeye tu ila tutacheza kitimu kuhakikisha tunafanikisha kile tunachokihitaji.”

Shida ya Argentina ni safu yao ya ulinzi. Kwa utabiri nadhani Mchezo huu unaweza kwenda kwa jumla ya mabao matatu kwa upande wa Argentine. Kwa mtazamo wangu kuhusu Messi huwa kuna wakati anakuwa na mchecheto jasa mechi ambazo anahitaji kufikia rekodi ya Ronaldo.

Siwezi kusema lolote kinyume cha uwezo wake kwani ni mchezaji aliyefunga mabao matano katika mabao 7 ya Argentina kwenye kombe la dunia hivyo siwezi kusema kama leo hatoweza kufunga.

Argentina imefungwa mchezo mmoja kati ya 7 dhidi ya timu za ulaya katika hatua ya makundi mwaka 2002 dhidi England, imetoka sare michezo miwili na kusshinda minne hivyo sioni Icelanda watatoka vipi hapa. Mchezo mwingine ni ule wa fainali dhidi ya Ujeruman 2014

Argentina

Argentina wamefuzu fainali za kombe la dunia mara 17, ikiwa ni mara 12 mfululizo. World Cup – and 12th in a row. Tokea mwaka 1978, ni ujerumani imeingia fainali mara tano huku Argentina wakifuzu mara 4.

Argentina wamefuzu hatua ya makundi mara 11 kati ya 12 ya mwisho, ukiondoa mwaka 2002 wameshinda mara 12 kayika michezo 15 na kipigo pekee walipokea mwaka 2002 dhidi ya England

Kwenye michuano hii wameshinda michezo yote ya mwanzo ya ufunguzi kwemye fainali tatu mfululizo.

Argentina wamekuwa naa msimu mbovu maana Bolivia ndiyo timu pekee iliyofunga magoli machache kuliko Argentine (18) Argentina wamefunga magoli (19) kwenye michuano ya kufuzu, Edinson Cavani amefunga magoli (10) magoli matatu zaidi ya Lionel Messi 7.

Iceland

Hii ni kwa mara yao ya pili kushiriki mashindano makubwa ukiondoa Euro 2016 bapo walifika hatua ya robo fainali. taifa hilo lina watu 334,000 na linaweka taifa dogo kabisa kuwahi kushiriki kombe la dunia. Gylfi Sigurdsson ndiye mfungaji bora akiwa na mabao 4.

Makala by Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here