Home Kimataifa Mambo usiyoyajua kuhusu kombe la dunia 2018

Mambo usiyoyajua kuhusu kombe la dunia 2018

10392
0
SHARE

Katika michuano ya mwaka huu ya kombe la dunia timu ya Panama ndio yenye wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji wake wakiwa na wastani wa miaka 30 na zaidi wastani ambao haujatofautiana sana na timu za Costa Rica, Ireland na Argentina ambao kwa pamoja wanaunda kundi la wahenga kwa mwaka huu jambo ambalo kwa Argentina linadhihirika zaidi kwa wachezaji wake nyota kama Lionel Messi, Aguero Dimaria, Mascherano na wengine ambao kila mmoja ana vuka miaka 30 kwenda mbele.

Kwa upande wa pili Nigeria ndio timu ya watoto unaweza kusema hii ni kutokana na wastani wa umri mdogo kwa timu zote zilizokwenda Urusi. Nigeria ina kikosi cha wachezaji wenye wastani wa miaka 24 wastani unaozidi kidogo ule wa Ujerumani na England timu zinazofuatia kwa udogo wa umri baada ya Nigeria wote wakiwa na wastani wa miaka 25.

Kwenye michezo inafahamika wachezaji wenye vimo virefu ndio wenye faida, wahispania hawaamini hili kwani wao ndio wenye kikosi chenye wachezaji wafupi kuliko vyote kwa wastani wa kimo sambamba na Peru, Argentina, Uruguay, Saudi Arabia, Mexico na Japan. Timu zote hizo zikiwa na wachezaji ambao kwa jumla yao wana wastani wa kimo cha chini ya cm 180 huku mataifa ya Denmark, Sweden, Ireland na Serbia yakiongoza kwa kimo kwa pamoja ambapo Serbia wanaongoza kwa jumla wakiwa na wastani wa zaidi ya cm 185 za urefu wa wachezaji wake jambo ambalo linadhihirishwa na kimo cha mtu kama Nemanja Matic.

Linapokuja suala la timu ya taifa dhana ya utaifa huwekwa mbele huku matarajio yakiwa ni kuona uzalendo unaotokana na mahaba aliyonayo mchezaji yanayotokana na taifa lake hasa inapokuwa amezaliwa katika taifa hilo. Kesi hii ni kinyume kwa Morocco ambao katika kikosi cha watu 23 ni watu sita pekee ambao ni wazaliwa wa Morocco wengine wakiwa wamezaliwa mataifa kama Uhispania, Ureno, Uholanzi na Ubelgiji.

Katika michuano ya mwaka huu kuna wachezaji wenye umri wa miaka 20 wakiongozwa na beki wa England Trent Alexander-Arnold kwenye orodha hiyo ndio mchezaji pekeake ambaye hajawahi kuichezea timu ya taifa kwenye mchezo rasmi wa kiushindani. Katika orodha hiyo mu-australia Daniel Azan ndio mwenye umri mdogo akiwa na umri wa miaka 19, miezi 5 na siku 10.

Kipa wa Nigeria Francis Uzoho ndiyo kipa mwenye umri mdogo katika orodha ya wakongwe Essam El-Hadary mwenye umri wa miaka 45 na miezi 5 akiwa pia mchezaji mwenye umri mkubwa kuliko wote na pia ndio nadhoha mkubwa kuliko wote kiumri, katika orodha ya manahodha Harry Kane wa England ndio nahodha mdogo kuliko wote akiwa na miaka 24 akizidiwa miaka 21 na Essam El-Hadary.

Nahodha wa Mexico Rafael Maques ndio mchezaji wa ndani mwenye umri mkubwa kuliko wote akiwa na miaka 39. Wastani wa umri ujumla wake kwenye michuano ya mwaka huu ni miaka 28 wastani ambao ni mkubwa kwenye historia ya michuano hii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here