Home Kimataifa Couples waenda honeymoon World Cup na bajeti ya mamilioni

Couples waenda honeymoon World Cup na bajeti ya mamilioni

9105
0
SHARE

Uzuri wa fainali za kombe la dunia lina mambo mengi sana ukiachana na mechi za uwanjani ndiyo maana watu wanaamua kutumia pesa kibao kuhakikisha wanakuwa sehemu ya historia ya mashindano haya.

Katika misele ya Shaffih Dauda ndani ya jiji la Moscow kuhakikisha msomaji wake anapata vitu adimu mara paaap anakutana na wapenzi wadogo kutoka Argentina.

Hapa ishu sio mapenzi yao ila ishu ni kilichowafanya wao kuwepo Urusi. Young couple kutoka Argentina wamesema wameoana siku si nyingi na kuamua ‘Honey Moon’ yao iwe World Cup.

Bajeti yao sasa ndiyo balaa, unaambiwa  mzigo waliopanga kutumia kwenye fainali za kombe la dunia 2018 unakaribia Argentine Peso 550,000 ($20,000) sawa na Tsh45,000,000.

Watakuwa Urusi kwa mwezi mzima waki-enjoy na kupata experienc ya kombe la dunia. Piga ua hawa watakua wametoka familia bora tu zile za ‘mom am going i need to use you car’ #FootballCouple

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here