Home World Cup URUSINI: Tathimini ya mchezo wa Morocco vs Iran

URUSINI: Tathimini ya mchezo wa Morocco vs Iran

8780
0
SHARE

Naam hii ndio Eid Mubaraka. Imekuja tofauti na mawazo ya wengi. Kwa bahati nzuri ulikuwa mpambano maustazi wa Kiran na wale kutoka milima ya Atlas Morocco. Kikosi cha Morocco kilijumuisha wachezaji 17 wa kigeni yaani waliozaliwa nje ya taifa lao, huku watano wakiwa wazaliwa wa Uholanzi.

Mpaka sasa mechi mbili bado timu za afrika hazijapata bao. Mambo yameenda ndivyo sivyo kwa Morocco. ikiwa zimesalia dakika 2 wamorocco wanaondoka na kilio uwanjani.

Kimsingi mchezo ulivutia sana. Kipindi cha kwanza Morocco walipiga mashuti 9 na kuweka rekodi yao ya kupiga mashuti mengi kwenye kombe la duniaa kwemye mchezo mmoja tokea mwaka 1994 kwenye mchezo dhidi ya Saudia Arabia.

Mchezo ulikuwa wa kasi sana na kila aliyetazaman mtanange huu alikuwa anaamini kwamba Morocco wataibuka washindi.

Kosa la Kwanza Herve Renhard amejiona mjuaji. Matumizi mabaya ya wachezaji. Hakim Ziyech ni kiungo wa katikati. Msimu huu akiwa kaama kiungo wa kati amefunga Magoli 9 na kutengeneza magoli 15. Akiwa kama winga hajafanya chochote zaidi ya kukimbia kimbia.

Herve amemweka Ziyech kama winga wa kushoto na kumweka Belhanda acheze nafasi ambayo Ziyech alikuwa wa muhimu zaidi. Belhanda amekuwa akitumika kama winga wa kulia au kiungo wa katikati. Ziyech alitumika kushoto na kumweka Harit kulia. Harit amekuwa akicheza winga wa kushoto kwa takriba michezo 10 kule Shackle je kwanini leo kulia? Ziyech amecheza michezo 30 kama kiungo mshambuliaji kwanini leo ampeleke kushoto?

Bila shaka mwalimu alitaka timu ipige mipira ya krosi tu ili kumtafuta El Kaarb. Kwa mfumo huu alibana uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kucheza sehemu anayoweza kufanya vyema.

Msshambuliaji Bouhoddaz aliingi Kumpokea Kaarb dakika za mwisho. Alikwenda kwa lengo la kufunga lakini kwa bahati mbaya akajifunga.

Tunaweza kusema ni siku mbaya kwa bara la Afrika. Morocco walipiga mashuti 13 huku Iran wakipiga. Huu ndio Ushindi wao wa pilo katika historia ya kombe la dunia. Ushindi wao wa kwanza ulikuwa mwaka 1998 dhidi ya Marekani. Morocco wanazidi kubaki na rekodi yao ya kutokushinda mchezo wao wowote wa ufunguzi. Mwenye asili haachi asili yake.

Kundi la Morocco ni gumu mno. Sioni kama kuna nafasi yoyote. Angalau mchezo wa leo wangeshinda kisha waombe Ureno na Hispania watoke suluhu. Kisha michezo miwili ijayo wapate suluhu kisha afungwe mmoja.

Sioni nafasi yao licha ya kwamba mpira hautabiriki.

Kimahesabu Morocco tumeshamalizana nao mahesabu. Wamepata mchezo mrahisi sana lakini mwisho wa siku wametuonesha kuwa hawana haja ya kuendelea kubakia mchezoni.

wapo watakaomlaumu aliyejifunga lakini tujiulize je muda wote walikuwa wapi hadi kuja kusubiri matatizo yatokee?

Makosa yale yale yaliyotokea mchezo wa Misri ndiyo hilo hilom. One mistake One goal. lipigalo lafunza. Labda Senegal naTunisia wanaweza kujifunza. Kufungwa goli moja sio tija. Je unafunga mangapi. Kama unafungwa goli baada ya takribani dakika 90 huo ni uzembe wa timu nzima. Hata kama matokeo yangebaki 0-0 bad tu Morocco bai bai.

Shida kubwa iliyoikumba Morocco ni muunganiko mzuri wa mawinga wa pembeni akina Belhanda na mshambuliaji wao wa Mwisho Al Kaab.

Morocco walifanikiwa kuumiliki mpira kwa asilimia 70 lakini katika hatua ya mwisho walikosa mbinu mbadala. Ndio walitengeneza nafasi lakini bado umaliziaji haukuwa na tija sana hasa ukilinganisha na uwezo waliouonesha kwenye dimba la kati.

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here