Home World Cup URUSINI: Je Ronaldo atafuta uteja?

URUSINI: Je Ronaldo atafuta uteja?

8101
0
SHARE

Jana tarehe 14 mwezi juni Fainali za kombe la Dunia zilifunguliwa na wenyeji Urusi wakipata ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Saudi Arabia ,Michezo mingine itapingwa leo mchezo wa mapema utakuwa saa 9 mchana kwa saa za afrika mashariki,Morroco dhidi ya Iran na baadae usiku ni the Iberian derby wababe wa ulaya magharibi wanakutana Hispania dhidi ya Ureno,

Shaffih Dauda atakuletea kila chembe ya tukio kule Urusi

Fainali ya kwanza itakuwa leo katika dimba Fisht Arena

Katika dimba la Fisht kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya mabingwa wa 2010 wa kombe la dunia Hispania dhidi ya Ureno,waatalamu wa historia wanautaja huu mchezo kuwa ni mchezo wa mahasimu (derby )ni moja ya derby kwa timu za taifa kwani ukiacha tu mpira Hispania na Ureno zinatokea eneo moja la ulaya yaani Ulaya magharibi ( lugha moja ), maeneo ya Iberian maana yake huu mchezo unaitwa mahasimu wa ulaya mgaharibi (Derby of Iberian ).

Kwa mara ya kwanza mchezo uliowakutanisha hawa wakubwa wawili ulikuwa mwaka 1921 Disemba 18,wakati Ureno walipoambulia kichapo cha goli 3-1 kutoka kwa Hispania ,mchezo wa pili ulikua mwaka 1926 mchezo uliisha sare ya 2-2,1947 Ureno walifuta uteja kwa hispania na kuwachapa 4-1 katika mchezo wa kirafiki jijini Lisbon.

Matokeo ya ajabu

Mwaka 1934 katika mchezo wa kombe la dunia kati ya Ureno dhidi ya Hispania ,Ureno walipokea kipigo cha paka mwizi cha magoli 9-0.

Hivyi karibuni

Ureno walifungwa 1-0 nchini Afrika kusini kwenye mchezo wa kombe la dunia goli la dakika ya 63 la David Villa lilifanya Hispania kukata ticketi ya kwenda robo fainali na baadae kuchukua kombe katika mchezo wa fainali dhidi ya Uholanzi goli la fainali likifungwa na Iniesta dakika za nyongeza.

Hispania dhidi ya Ureno walikutana tena katika mashindano ya Ulaya kwa ngazi ya timu za taifa yaani (Uefa euro )jijini Donestk nchini Ukrine na Ureno akambulia kipigo kwa mikwaju ya penati 2-4..

Jumla ya Hispania na Ureno wamecheza michezo 36 ,Hispania wameshinda mara 18,Ureno mara 12 na Sare 6.

Je Ureno atafuta uteja dhidi ya Hispania

khalidchukuchuku

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here