Home Kimataifa Mambo na vijimambo ufunguzi kombe la dunia 2018

Mambo na vijimambo ufunguzi kombe la dunia 2018

8655
0
SHARE

Mechi ya ufunguzi kati ya mwenyeji Urusi na Saudi Arabia ilishuhudia mwenyeji Urusi ikishinda 5-0 lakini kuna vijimambo ambavyo vilikuwa vinaendelea nje ya pitch ambavyo huenda uliona baadhi na vingine vilikupita.

Kuna picha ambayo ime-trend sana ikimuonesha mfalme mtarajiwa wa Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman pamoja na Rais wa Urus Vladimir Putin na katikati yao alikuwepo Rais wa FIFA Gianni Infantino picha hii ilionesha wakuu wa mamlaka tatu (mkuu wa taifa la Urusi, mfalme mtarajiwa wa Saudi Arabia na mkuu wa mchezo wa mpira wa miguu). Picha hii inaonesha nguvu ya mchezo wa soka kwamba watu wengi wanaufurahia.

Prince Salman na Rais Putin wa Urusi walikuwa wamekaa pamoja katikati yao alikaa Rais wa FIFA Infantino, baada ya goli la kwanza Mfalme wa Saudi Arabia alimuinamia Putin akampa mkono lakini kadiri magoli yalivyokuwa yanaongezeka Mfalme akawa mpole.

Mfumo wa kutumia waamuzi wa nje ya uwanja hasa wale ambao wanasaidiwa na television (VAR), kwa kawaida kwenye TV za uwanjani huwa yanatokea majina ya wachezaji watakaoshiriki mchezo husika halafu baadayeyanatokea majina ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo.

Mara nyingi tumezoea kuona majina ya waamuzi wanne lakini katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia 2018 ilikuwa tofauti, katika mchezo huo yalionekana majina ya waamuzi 11.

Waamuzi wanne ni wale wa msingi (mwamuzi wa kati, wawili wa pembeni na fourth official) na wengine saba ambao wanakaa kwenye chumba cha TV.

Msanii Robby Williams kutoka England alikuwa anatajwa kwamba kuna utata ambao unaweza kuibuka kwa sababu kuna wimbo ambao aliutoa mwaka 2016 una maneno yasiyofaa kuhusiana na Urusi kama taifa lakini katika performance ya ufunguzi hakuimba wimbo huo.

Mbali na kutotumbuiza wimbo huo Williams alionesha ishara ya kidole cha kati kwenye moja ya camera ambazo zilikuwa zinafuatilia tukio la sherehe za uzinduzi, kitendo ambacho kimelaaniwa na watu wengi  na kukiona cha kihuni.

Ukiachilia mbali mechi za uwanjani watu wengi huwa wanavutiwa na sherehe za uzinduzi au ufungaji wa kombe la dunia kwa hiyo kitendo kilichofanywa na Williams kilitia doa sherehe za ufunguzi.

Kombe la dunia likawakutanisha Jose Mourinho na legend wa Argentina Javier Zanetti kwenye uwanja wa Luzhniki wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya mwaka huu.

Wawili hao wali-pose kwa picha na baadaye Zanetti akaandika kwenye ukurasa wake wa instagram: “Ni special kukutana na wewe Jose.”

Zanetti alikuwa nahodha wa Mourinho wakati Inter inashinda vikombe vitatu (treble) mwaka 2010. Serie A, Coppa Italia pamoja na Champions League.

Baada ya kukaa na mfalme mtarajiwa wa Saudi Arabia kwenye eneo la VIP Rais wa Urusi Vladimir Putin baada ya game alisimama kupiga picha na boss wa Manchester United Jose Mourinho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here