Home Kimataifa Kumchukia Cr7 ni kujitesa, apiga hattrick ya kwanza kombe la dunia

Kumchukia Cr7 ni kujitesa, apiga hattrick ya kwanza kombe la dunia

20058
0
SHARE

Ilimchukua Cristiano Ronaldo dakika 4 kuiandikia Ureno bao la kwanza kwa mkwaju wa penati, bao hili limemfanya Cr7 kuungana na Pele, Miroslav Klose na Uwe Seeler kama wachezaji waliofunga katika michuano minne tofauti ya kombe la dunia.

Lakini dakika ya 24 Diego Costa alipiga shuti lake la kwanza on target katika kombe la dunia na akafanikiwa kufunga, kabla ya Cr7 dakika ya 44 kufunga bao la pili na kumfanya kufunga mara mbili katika shot on target 3 siku ya leo.

Dakika ya 55 tena Diego Costa aliufanya mchezo kuwa 2-2, lakini Ureno wakiwa bado hawaamini lilipigwa shuti la kushtukiza nje ya box na kuipa Hispania bao la 3, na kuwa mchezaji wa pili kuifungia Hispania goli kwenye kombe la dunia akiwa nje ya box baada ya Fernando Hierro 1998.

Dakika ya 88 wakati mashabiki wa Hispania wakiamini wameshaokota alama 3, Cristiano Ronaldo mchezaji bora wa dunia kwa mara nyingine akaonesha kwamba yeye ndiye bora duniani kwa sasa baada ya kufunga bao la tatu na hii ikiwa hattrick yake ya kwanza katika michuano hii.

Hattrick ya leo inamfanya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kufunga katika kombe la dunia, hii leo Ronaldo alikuwa na miaka 33 na siku 130.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here