Home Kimataifa #VitukovyaUrusi, baada ya pweza mwaka 2010, safari hii ni paka kiziwi

#VitukovyaUrusi, baada ya pweza mwaka 2010, safari hii ni paka kiziwi

10931
0
SHARE

Mwaka 2010 katika fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini kulikuwa na pweza aliyefahamika kwa jina la Paul The Octpus, pweza huyu alifanya utabiri wa mechi nyingi ikiwemo ushindi wa Hispania.

Safari hii sasa nchini Urusi kuna paka ambaye ni kiziwi afahamikaye kama Achilles, huyu kazi yake iko kama Paul The Octpus ambapo anaonekana mtabiri wa michuano hii na tayari ameshaanza utabiri wake kwa mechi ya leo.

Inasemekana hapo kabla paka huyu alikuwa na kazi moja tu ya kudeal na panya kabla ya kugundulika kwamba anaweza kutumika kufanya utabiri wa michezo ya kombe la dunia 2018.

Kwa kuanzia katika mchezo wa leo kati ya wenyeji Urusi watakaokipiga dhidi ya Saudi Arabia, Achilles mwenye rangi nyeupe ametupa karata yake kwa Urusi na kuwatabiria kwamba ndio wataanza michuano hii kwa ushindi.

Achilles sio wa kumchukulia poa kwani hii sio mara yake ya kwanza kujaribiwa kufanya utabiri, katika michuano ya mabara nchini Urusi alitabiri mapemaa kwamba Ujerumani wangeshinda kombe hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here