Home World Cup URUSINI: Ramos vs Ronaldo, taarifa zote muhimu za Ureno vs Hispania

URUSINI: Ramos vs Ronaldo, taarifa zote muhimu za Ureno vs Hispania

10615
0
SHARE

Mpambano huu utapigwa kayika kiwanja cha Fisht Olympic Stadium kule Sochi.
Wachezaji wanne wa kocha mkuu wa Ureno Bwana Fernando Santos wamevunja mikataba yao na klabu ya Sporting Lisbon baada ya msimu wa kusuasua.

William Carvalho, Gelson Martins, Bruno Fernandes na Bas Dost waliungana na Rui Patricio and Daniel Podence walifungua jalada lao wakitaka kulipwa hela zao.

Swali ambalo ningetamani kumuuliza Hassani Kessy ambaye aliniambia kwamba yeye ataishabikia timu ya wapiga pasi na yenye beki katili, je Fernando Hierro atakamilisha safari yao?
Cristiano Ronaldo bila shaka huu ni wakati wake wa kuwatambia Pele na Maradona. Ureno haiwajahi kubeba kombe la dunia. Waliwahi kuwa na mchezaji bora kama Eusebio lakini mambo yalikwenda Mrama.

Ronaldo akili yake ni kujenga CV yake kubwa duniani wala sio kuhusu mkataba wake na Madrid.

Inahitaji moyo wa ziada kuamini kwamba Ureno inaweza kutwaa ubingwa dunia hata kama ina Ronaldo.

Hata hivyo rafiki yangu Hassan Masinde anaamini Ureno inaweza kuishangaza Hispania na dunia kwa ujumla kama ilivyofanya kule ufaransa miaka miwili iliyopita.

Ronaldo ana miaka 33 sasa. Si haba hasa kwa uwezo wake mkubwa alio nao. Bado ana uwezekano mkubwa. Mchezo wa huu kwake ni kamari. Kushinda kwake kutatoa onyo kwa wale mabingwa wengine. Ni ngumu kuamini kama Ronaldo atacheza kombr la dunia Qatar mwaka 2022.Hivyo kila mchezo kwake katika michuano hii ni sawa na fainali.

Kila ombi la Muargentina ni kuiombea Ureno ifungwe.
Waargentina wapo tayari kuona Saudia Arabia au hata Panama kubeba ubingwa wa dunia kuliko Ureno. Kama Ronaldo atabeba medali hii ya dhahabu niamini mimi hakuna mshabiki wa Messi atakayethubutu kufungua mdomo na kuongea chochote mbele ya mashabiki wa Ronaldo.

Tunafahamu kuwa Ramos ni Swahiba mkubwa wa Ronaldo. Sina shaka na utendaji kazi wao. Wala siamini kama Ramos atacheza chini ha kiwanfo ili swahiba wake azidi kumpa nafasi Ronaldo ya kufanya vyema zaidi kuliko Mess. Bila Shaka Ramos atahitaji kujenga rekodi yake. Yeye ni nahodha wa timu ya taifa. Hawezi kuleta usela kazini.

Karata yangu ni ipi?
La Roja walifanya maajabu mwaka 2010, Ureno nao walitwaa kombe la ulaya mwaka 2016. Yaani tunaweza kusema kwamba Wareno ile harufu harufu ya pilau lao la ubingwa mwaka jana baso wanalo. Tunaweza kusema hata yale masufuria bado hawajayaosha.

Ureno wapoje

Kwangu naona kama Ireno walishinda uchaguzi wa ubunge na kiabarua ni huu uchaguzi wa Uraisi. Ule Uchaguzi wa Ubunge hawakupewa nafasi kubwa ya kushinda lakini waliwashangaza wafaransa.

Fernando Santos anna uzoefu mkubwa kwani tayari amewahi kuvifundisha vilabu vya Porto, Benfica na Sporting Lisbon , na amepoteza michezo miwili tu kati ya 29 ukijuisha ushindi wa Chile kwa mikwaju ya penati kwenye kombe la shirrkissho la fifa. Kichapo kikubwa cha hivi karibuni kilitoka kwa Switzerland. Ureno imefunga magoli 32 na kuruhusu magoli manne katika michezo 10 ya mwisho.

Msururu wa Matokeo: DWLDDW

Kocha mkuu wa ureno

Hispania nao Vipi?

“Nimemsikia Hierro amesema hakuna muda wa kupoteza kupeana pole wala kulaumiana.

Je kuna faida yeyote kwa kocha wao Mpya?

Ndio, ila ndogo sana. Kwanza Hierro ni mzoefu na ni mhispania. Anaijua Hispania pamoja na ligi kwa ujumla. Amekuwa mkurugenzi wa Ufundi wa soka la timu ya taifa.

Changamoto ni kwamba hajawahi kuwa kocha wa timu kubwa au mashindano makubwa. Sio mbaya sana Maana hata Zidane alishtukiziwa kazi na hakuwahi kuwa kocha mkubwa hapo awali lakini alifanya makubwa.

Ramos amesema haoni kama kuna sababu ya kuangalia kama Hierro anafaa au hafai maana haoni ambaye anafaa zaidi ya Hierro ambaye yupo sokoni kwa sasa. Hakuna muda wa kupoteza.

Nimewaambia wachezaji kuwa wameshafanya makubwa na kazi iliyobakia mbele yao ni kuwekeza zaidi kwa kile kilichwapeleka Urusi.”

Fernando Hierro, ameifundisha tu Oviedo, na amepewa La Roja. Nimeangalia kwa makini uchambuzi wa Daniel Lewis, yeye amesema Hierro amepewa mzigo mkubwa sana kwenye lori Amepewa kikundi cha wachezaji bora duniani huku uzoefu wake yeyeni dereva taksi
Kimsingi hakuna timu yenye ulinzi Imara kama timu ya taifa ya hispania. Wakiwa wamefunga mabao 36 huku wakishikilia rekod ya kucheza michezo 20 bila kufungwa. Je Ureno watavunja chungu?

Msururu wa Matokeo: WDDWDW

Taarifa za timu
Dani Carvajal, bado ana wasiwasi kuanza kwemye mchezo huu. Kinda Alvaro Odriozola ambaye amecheza michezo 4 kwa timu yake ya taifa huenda akapewa mafasi ya kuziba pengo lake.

Ufundi.
Hierro atakuwa na uchaguzi mpana zaidi kati ya Andres Iniesta na Sergio Busquets kuanza kama viungo wa kati. Atakuwa na akiba ya Thiago Alcantara au Koke,

Santos kwa wachezaji wake wawili Goncalo Guedes na Bruno Fernandes.

Fernandes anaweza kuwa na Pepe kuhakikisha safu yao ya ulinzi inaimarika. Guedes atapata upinzani kutoka kwa Andre Silva ambaye amekuwa na uelewano mzuri na Ronaldo. Ronaldo ndiye mchezaji hatari zaidi katika mpambano huu akiwa amefunga mabao 81 kwenye michezo 150 ya kimataifa. Magoli 15 akiwa amefunga katika hatua ya kufuzu, huku msimu huu akitenga mabao mengine 43 kwa Real Madrid msimuu huu.

UTABIRI WA KIKOSI: URENO
Patricio; Soares, Pepe, Fernandes, Guerreiro; B.Silva, Carvalho, Joao Mario, Martins; Ronaldo, Silva

UTABIRI WA KIKOSI:UHISPANIA
De Gea; Odriozola, Pique, Ramos, Alba; Alcantara, Busquets, Iniesta; Isco, Costa, Silva

Makalla hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo. Utabiri wangu kuna uwezekano mkubwa sana suluhu licha ya kwamba naipa nafasi kubHispania zaidi ya ushindi kuliko Ureno.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here