Home Kimataifa Urusi vs Saudi Arabia wanatufungulia pazia la kombe la Dunia 2018

Urusi vs Saudi Arabia wanatufungulia pazia la kombe la Dunia 2018

8932
0
SHARE

Ilikuwa miaka minne, ikabaki mitatu, miwili, mmoja zikabaki siku na hatimaye hii leo kombe la dunia mwaka 2018 linaanza, wenyeji Urusi watafungua michezo hii wakikipiga dhidi ya Saudi Arabia.

Wasaudi Arabia wenyewe wameshasema wanajua kila mtu anawaza nini kuhusu wao lakini akasisitiza kwamba leo watawafunga Urusi kama asemavyo kocha wao Antonio Pizzi “tutawafunga Urusi na hii ndio nia yetu”

Lakini rekodi za michuano ya kombe la dunia zinaweza kuwa kikwazo kwa Waarabu hawa, hakuna timu mwenyeji ambayo imewahi kupoteza katika mechi ya ufunguzi, katika mechi tisa zilizopita waandaaji wa kombe la dunia walishinda 6 na suluhu 3.

Mnamo mwaka 1993 timu hizi mbili zilikutana japo mchezo huu haukua wa mashindano yoyote bali ulikuwa mchezo wa kirafiki ambapo Saudi Arabia waliifunga Urusi kwa mabao 4-3 na tangu hapo hawakukutana tena.

Warusi wana rekodi mbili (nzuri na mbovu) wanazofukuzia msimu huu, moja wanaweza kuweka rekodi ya Ufaransa 1998 ambao walikua timu ya mwisho kuwahi kuandaa michuano hii na kubeba ndoo au rekodi ya Afrika Kusini 1998 ya kuandaa michuano na kutolewa katika makundi.

Lakini kinachoogopesha kuhusu Urusi ni kwamba katika mara tatu walizoenda kombe la dunia 1994, 2002 na 2014 walishindwa kufudhu kwenda hatua ya mtoano na michuano yote hii wakimaliza nafasi ya 3 katika kundi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here