Home Kimataifa Mkwanja watakaoingiza FIFA kombe la dunia kufanyikia USA, Canada na Mexico

Mkwanja watakaoingiza FIFA kombe la dunia kufanyikia USA, Canada na Mexico

8267
0
SHARE

Story zinazohusu kombe la dunia ambazo zili-make headline jana ni Rais wa chama cha soka cha Hispania kumtimua kocha wao wa timu ya Julen Lopetegui baada ya kupata taarifa muda mfupi kabla ya Real Madrid kumtangaza kocha huyo kuwa kocha wao mpya kuanzia msimu ujao.

Ishu nyingine ni kuhusu umoja wa mataifa ya Marekani, Canada na Mexico kupewa uenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026.

Mataifa mengi ya Afrika yalikuwa na imani Morocco itapewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2026 lakini katika mkutano mkuu ambao umefanyika Moscow wakati mataifa yanayowania nafasi hiyo yakifanya presentation ya namna watakavyo andaa mashindano, wadau wengi walibadilika kutokana na presentation ya mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.

Mataifa hayo matatu ambayo yalikuwa yanaonesha kwamba, pamoja na fainali kufanyika 2026 lakini viwanja ambavyo vitachezewa mashindanovyote vimekamilika sio hadi ifike 2026 ndio waanze kukarabati na kujenga lakini hata wakipewa fursa ya ku-host mashindano haya ya Urusi wako tayari kwenye upande wa viwanja.

Kingine ambacho kimewapa faida ya kuchaguliwa kuwa wenyeji wa mashindano ni kwamba, wakati wanaonesha faida ambazo FIFA na wanachama wake watazipata kutokana na tiketi zitakazouzwa, tayari dola za Marekani 2 Billion ni faida ambayo FIFA itatengeneza wakati kwa morocco ilikuwa inaonekana wangeuza dola 1 Billion.

Kiasi ambacho FIFA watatengeneza kama kodi ni dola 14 Billion iwapo Marekani, Canada na Mexico watapewa nafasi ya uenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa hiyo dola 14 Billion ni faida kwa FIFA tofauti na Morocco ambao kwenye presentation yao wameonesha kwamba ili waweze ku-host fainali za kombe la dunia za 2026 viwanja 16 ambavyo walivianisha kwamba vitatumika wakati wa mashindano vyote havijakamilika baadhi vinahitaji kujengwa na vingine vikihitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Kingine kilichowaangusha Morocco ni kwamba, wanahitaji kuwekeza dola 16 Billion kwenye kutengeneza miundombinu na kufanya matayarisho mengine. Kwa hiyo presentation yao dhidi ya Marekani, Canada na Mexico moja kwa moja iliwafanya wajumbe wa mkutano mkuu waone wakifanya kosa kuipigia kura Morocco wanaweza kuumia mbele ya safari ndiyo maana Marekani ikapata kura nyingi na kuibuka mshindi.

Katika mechi 80 ambazo zitachezwa kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2026 kutokana na ongezeko la timu hadi kufikia 48, mechi 60 zitafanyika Marekani, mechi 10 Canada na mechi 10 nyingine zitachezwa Mexico.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here