Home Kimataifa Kipigo walichotoa Urusi chaweka rekodi hizi kombe la dunia

Kipigo walichotoa Urusi chaweka rekodi hizi kombe la dunia

9165
1
SHARE

Mwaka 1974 wakati Italia wakiandaa michuano ya kombe la dunia, mechi ya ufunguzi walikutana na USA ambapo walidondosha kipigo cha mabao 7-1 ikawa rekodi kubwa kwa timu mwenyeji kutoa katika mechi ya ufunguzi.

Hii leo waandaaji wa kombe la dunia mwaka 2018 timu ya taifa ya Urusi wametoa dozi nene kwa kuichapa Saudi Arabia mabao 5-0  na hii inakuwa mechi ya pili kwa mwenyeji kutoa kipigo katika pambano la ufunguzi tangu 1934.

Mara ya mwisho kwa timu ya taifa ya Urusi kufunga mabao 3+ ilikuwa mwaka 1994, hii pia ilikuwa katika michuano ya kombe la dunia ambapo Urusi waliichapa timu ya taifa ya Cameroon kwa mabao 6-1.

Yuri Gazinskiy ndiye alikua wa kwanza kufunga kwa Urusi na sasa anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika kombe la dunia 2018, Yuri sasa anakuwa mchezaji wa pili kufunga kwa shuti la kwanza on target tangu Philip Lahm afanye hivyo 2006.

Denis Cheryshev aliingia dakika ya 24 na kufunga bao dakika ya 43 na hii inamuweka katika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufunga katika mchezo wa ufunguzi huku akitokea benchi.

Sergei Ignashevic ambaye leo aliichezea Urusi amevunja rekodi ya Roger Milla ya mwaka 1994 ambaye alikuwa mchezaji mzee kucheza kombe la dunia, Sergei leo alicheza mechi hii akiwa na miaka 38 na siku 338 hii ikiwa rekodi ya mchezaji mzee kuwahi kushiriki kombe la dunia.

Comments

comments

1 COMMENT

  1. mwaka 1974 fainali za kombe la dunia zilifanyika Ujeremani siyo Italia(Mwaka 1974 wakati Italia wakiandaa michuano ya kombe la dunia) paragrafu ya mwanzo

    Pili Roger Milla alicheza kombe la dunia mwaka 1994 Marekani akiwa na umri wa miaka 40 kwa hiyo Sergei Ignashevic wa Urusi hajavunja rekodi hiyo tafadhari rekebisha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here