Home Ndondo Cup UV TMK kwenye mikono ya Juma Kaseja

UV TMK kwenye mikono ya Juma Kaseja

8406
0
SHARE
Kutoka Kinesi Jana timu ya Umoja wa Vijana Temeke wameshinda mabao matatu kwa bila dhidi ya stim tosha. Rashid Juma aliyejitwalia tuzo ya mchezaji chipukizi wa simba aliifungia UV TmK mabao mawili huku akiwa kivutio katika mtanange huo hasa bao lake alilofunga umbali wa takribani Mita 20 na kumshinda mlinda mlango wa Stim Tosha Mustapha Mabruki.

Mpira ulikuwa wa kasi sana. Stim tosha ilikuwa chini ya Kelvin Kiduku ambaye baada ya mchezo alihimiza mashabiki na viongozi kuyakubali matokeo na kujioanga upya. Dimba katikati kwa upande wa UV TMK lilitawaliwa na kiungo mwenye udambwi Gerald Adam pamoja na kiungo chipukizi wa Azam Abbas Kapombe.

Pia Masoud Nassoro Cholo alisimamia safu ya Ulinzi ya UV TMK. TMK walionekana kutawala mchezo kwani wachezaji walitulia vyema uwanjani. Baadae kiungo Machachari God Wambura aliinia kumpokea Gerald.

Juma Kaseja alionekana kuwa kivutia kikubwa uwanjani hasa baada ya kuonekana katika michuano huo akiwa mlinda mlango wa UV TMK.

Makelele ya Mashabiki wengi yalikusa uwanjani hasa wakionesha kushangazwa kwao kwa mchezaji huyo kucheza ndondo. Tulipata bahati ya kufanya nae mahojiano nae alituambia kwamba hii ni mara yake ya kwanza kucheza michuano kama hii. Shida kubwa aliyoiona hapa ni changamoto ya uwanja.

Vijana wengi wana uwezo lakini uwanja huu unawanyima nafasi wachezaji wenye uwezo kuonesha vipaji vyao

Kuna watu walionekana kumtusi kaseja. Bila shaka sioni tatizo la Kaseja kucheza michezo hii maana anakuja pia kutia hamasa na kuvuta mwamko wa mashabiki na vijana wadogo. Wapo wachezaji wakubwa tu dunia wameenda ligi za mchangani hasa baada ya viwango vyoa kupungua au kukumbwa na uzee. Wapo watu kama akina Tevez, Xavi na wengineo wengi ambao kwa sasa wapo ligi ndogo.

Kaseja amekuja kutia hamasa. Wapo watu hawamjui na wanatamani kumuona hivyl anakuwa kivutia kikubwa. Pia uwepo wake yeye kama mchezaji mkongwe kunaongeza chachu kwa vijana wadogo. Uwepo wake pia ni msaada kwa timu husika hasa kimbinu na anawatia moyo vijana n.k

Tulipomuuliza kuhusu nafasi ya TMK kutwaa Ubingwa alisema.

Ukiitazama timu yetu kwa harakaharaka huwezi kuipa nafasi. Lakini mafanikio ni kujipanga na umoja. Timu yetu nina amini itafanya vizuri. Mchezo wa leo umetoa mwanga hasa kwamba sisi ni timu ya aina gani

Rashid Ali mchezaji chipukizi wa Simba nae alisema yupo Ndondo kwa ajili ya kujinoa zaidi na anaamin kuwa Tuzp ile itampa nguvu na hamasa kubwa zaidi.

Pia huu ni ujio mpya wa Wambura ambaye amekuwa akikumbwa sana na majerahaara kadhaa hasa katika michezo ya ligi kuu. huenda ni wasaa mwingine wa yeye kujinoa upya na kurudi tena upya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here