Home Kimataifa Morocco walivyopigwa kikumbo na USA kuandaa kombe la dunia

Morocco walivyopigwa kikumbo na USA kuandaa kombe la dunia

8618
0
SHARE

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye hii leo nchi za Canada, USA na Mexico zimeshinda dhabuni ya kuandaa michuano ya kombe la dunia na kulinyima bara la Afrika kuandaa michuano hii kwa mara ya pili.

Kama hufahamu ni kwamba Mexico sasa wanaingia katika vitabu vya rekodi kwa kuwa taifa la kwanza kuandaa michuano hii mara tatu, huku USA bado wana rekodi ya kuwa na idadi kubwa ya mashabiki kuangalia kombe la dunia ilikuwa mashabiki mil 3.6 mwaka 1994.

Wakati nchi hizi zikitangazwa kushinda kuandaa michuano hii, raisi wa chama cha soka cha Marekani Carlos Cardeiro alionekana kububujikwa na machozi kutokana na nchi yake kushinda hili.

Si kwamba Cardeiro alikuwa haamini kinachotokea bali yalikuwa machozi ya ushindi, Cardeiro amekiri kwamba amelia kwa ajili ya mataifa haya na umoja ambao timu yao iliyokuwa ikipambania jambo hili lililofanikiwa.

Morocco walionekana kuwa na support kubwa sana kutoka Afrika na wakagawana Asia, na Cardeiro alilifahamu hilo na wao wakaliona bara la Ulaya kama sehemu kubwa ambapo wangefanya ushawishi kushinda kura nyingi.

Cardeiro anasema yeye ni mtu wa familia na wakati wote yuko na familia yake lakini miezi mitatu ya mwisho kabla ya siku ya leo walizunguka kila mahala wanapojua wanaweza kupata kura na hii ilimfanya kuwahi kulala kwake katika siku 10/90 tu ndani ya miezi hii mitatu.

Kambi ya Cardeiro pamoja na wenzake ilihamia London na waliweka makazi hapo kujaribu kuzungumza na wanachama wa FIFA na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani hata Urusi ambao walikuwa wakiisuport Morocco walishawishika na idea za Cardeiro na wenzake na kubadili muelekeo.

Ukiacha bara la Afrika ambako ilikuwa ngome kubwa ya Moroco, USA walipata kura 33/46 katika bara la Asia, wakaja wakapata kura 41/55 katika bara la Ulaya lakini hata bara la Afrika waliokota kura 11 kati ya kura 54.

Hii itakuwa michuano ya kwanza ya kombe la dunia ambayo itakuwa na timu 48 badala ya 32 za sasa, na miji 16 kutapigwa mitanange ya kombe la dunia 2026 na zitachezwa jumla ya mechi 84.

Michuano hii inaonekana itaifaidisha zaidi USA kuliko Mexico na Canada, kwani achilia mbali fainali kupigwa kwao lakini wao ndio wana viwanja vingi zaidi 17, na michezo 60/80 itapigwa katika viwanja vyao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here