Home Kimataifa Mshambuliaji anayetajwa Simba amtabiria Lukaku kutwaa kiatu cha dhahabu

Mshambuliaji anayetajwa Simba amtabiria Lukaku kutwaa kiatu cha dhahabu

11235
0
SHARE

Kombe la dunia hili hapa linaanza huku Ndondo Cup nayo moto unaendelea kuwaka pale Kinesi na Bandari. Hii leo katika uwanja wa Kinesi timu ya Faru Fc waliichapa East Zuu bao 2-0 na kuanza michuano hii vyema.


Katika kikosi cha Faru Jeuri Fc hii leo kikiongozwa na Athumani Iddi Chuji lakini upande wao wa kulia alikuwepo Awesu Awesu nyota wa Mwadui ambaye alikuwepo katika majina 30 ya mwanzo ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora VPL.

Awesu Awesu ambaye alikua kwenye rada za Simba tangu akiichezea klabu ya Madini Fc na sasa anaitumikia Mwadui Fc humuambii kitu kuhusu kombe la Dunia, Awesu anasema yeye ni Hispania mwanzo mwisho na anaamini japo kocha wao Julen Lupetgui amefukuzwa.

Lakini pamoja na kuitabiria Hispania kuwa mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2018, Awesu anaamini kwamba mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku ndiye atakayeibuka ni kiatu cha mfungaji bora wa michuano.

Katika michezo 9 iliyopita ambayo Lukaku ameitumikia timu ya taifa ya Ubelgiji amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 13 huku akifanikiwa kuassist mar 3  na hii inamfanya kuhusika katika mabao 16 katika mechi 9 zilizopita za Ubelgiji.

Awesu anaamini kiwango ambacho Lukaku anakionesha katika timu ya taifa ni tishio sana kwa mabeki na itakuwa ngumu wengi kumzuia, Awesu amesisitiza kwamba hata Hispania wenyewe wanaweza kupata ugumu kumzuia Lukaku na ndio maana anaiona Ubelgiji kama tishio kubwa kwa Hispania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here