Home Kitaifa Kwa mara ya kwanza Kaseja Ndondo Cup

Kwa mara ya kwanza Kaseja Ndondo Cup

8951
0
SHARE

Kwa sasa ukimtaja Juma Kaseja mashabiki wa soka wanakumbuka alivyopangua mkwaju wa penati ya Okwi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba siku ambayo ‘mnyama’ alivunjiwa rekodi yake ya kutopoteza mchezo VPL baada ya kufungwa 1-0 na Kagera Sugar.

Ukiachana na ukongwe wote na heshima aliyoweka Kaseja ndani na nje ya soka la Tanzania, alikuwa hajawahi kucheza mechi za Sports Xtra Ndondo Cup lakini kwa mara ya kwanza alikaa kwenye milingoti ya magoli ya Ndondo Cup kuidakia UV TMK ilipocheza dhidi ya Stim Tosha ‘Stamala’.

“Nilikuwa sijawahi kucheza mashindano ya Ndondo, hii ni mara yangu ya kwanza nacheza. Mashindano hako poa na yanasaidia vijana kuonekana na kuwajengea uzoefu kwa sababu huku wanakutana na wachezaji wengi wenye uzoefu na mbinu nyingi”-Juma Kaseja.

Kaseja aliiongoza UV TMK kushinda 3-0 dhidi ya Stim Tosha katika mchezo wake wa kwanza Ndondo Cup.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here