Home Kimataifa Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakutanishwa Russia na F4F

Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakutanishwa Russia na F4F

9008
0
SHARE
Gazprom Football for Friendship 2018 watajumuisha watoto kutoka mataifa 211 kote duniani. Gazprom Football for Friendship
Kutoka: MOSCOW

2018 Football for Friendship (F4F)dro hii imefanyika katika jiji la Moscow. F4F ni mfuko wa pamoja wa watoto kote duniani ulioandaliwa na kampuni ya Gazprom ambaye ni mbia wa FIFA kwenye maandalizi ya Kombe la Dunia kule Russia mwaka 2018.

Lengo kubwa kubwa ni kutoa fursa kwa vijana wadogo wanaochipukia kwa vipaji mbalimbali na kuinua talaanta zao. Shirikisho hili la watoto lina lengo la kuweka umoja, ushirkiano, urafiki na kubadilisha tamaduni mbalimbali.

Tukio la mwisho litafanyika Moscow, Russia, 8-15 June 2018.

Kutakuwepo na timu 32 za kimataifa zitakazoundwa kwa mfumo wa uchezaji wa kawaida kabisa uwanjani kutokana na kipaji cha kila mchezaji kutoka kila taifa. (Mlinda lango, Walinzi, Viungo na washambuliaji) .

Mashindano haya yatafanyika kwa kuangalia
jinsia, Umri, na Ulemavu. Umri wao haupaswi kuzidi miaka 12. Kila timu kutoka kila nchi itaongozwa na makocha wasiozidi umri wa miaka 14-16

Vyombo vya habari zaidi ya 5000 vitahussika kurusha matangazo hayo mubashara. Mkutano wao mkuu utafanywa na watoto wadogo ambao wana vipaji vya kuwa waandishi wa habari ambao hawapaswi kuzidi umri wa miaka 12 kutoka mataifa yote husika. Watoto wote walioteuliwa watakuwa mabalozi katika nchi zao.

Vijana wawili wa kitanzania ambao wamepata

bahati ya kuiwakilisha Tanzania katika

michuano hiyo, Zipora Mollel pamoja na

Laigwanani Lomayani Mollel ndio

wamechaguliwa na Football for Friendship (F4F).

Hawa ndip mabalozi wa F4F walioshiriki tukio la ufunguzi: Zahar Badyuk (Russia), Runqi Cui (China), Juan Manuel Pinola Silveira(Uruguay), Lilya Matsumoto (Japan),Ananya Kamboj (India), Christopher Sowah Mensah (Ghana).

Mwenyekiti wa PJSC Gazprom Mr. Victor Zubkov, Katibu mku wa FIFA General Bi. Fatma Samoura, Mshindi wa tuzo za Olympic Bi. Adelina Sotnikova, mshindi wa ragamata mbili kutoka Russia, Mshindi wa raga michuano ambaye amekuwa akitumia viti. Ya walemavu Mr. Yuri Kamenets, Legendari wa mpira wa Mr. Marco van Basten walihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba zao.

Programu ya Football for Friendship (F4F) 2018 inabadilisha ndoto ya kombe la Dunia la FIFA kuwa kweli kwa Zipora Mollel pamoja na Laigwanani Lomayani Mollel, vijana hao kutoka kabila la Maasai wamechaguliwa kwenda Russia kuiwakilisha Tanzania huku gharama zote zikibebwa na F4F.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here