Home Kitaifa Mshindi wa tuzo ya Mo Simba Awards atupia mbili Ndondo Cup

Mshindi wa tuzo ya Mo Simba Awards atupia mbili Ndondo Cup

10703
0
SHARE

Michezo ya Ndondo Cup hatua ya makundi imeendelea leo Jumanne June 12, 2018 kwa mechi mbili kuchezwa viwanja tofauti. Uwanja wa Chuo cha Utalii Tanzania ‘Bandari’ Kauzu imenza vyema kwa ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Tandika Kombaini.

Cliff Anthony wa Kauzu amefanikiwa kuchaguliwa Man of the Match katika mchezo wa Kauzu dhidi ya Tandika Kombaini.

Uwanja wa Kinesi Stim Tosha imeanza vibaya mashindano baada ya kufungwa 3-0 dhidi ya UV Temeke.

Mshindi wa tuzo ya mchezani bora kijana ya Mo Somba Awards 2018 Rashid Juma amefunga magoli mawili kati ya matatu Katik mchezo huo.

“Temeke ni sehemu ambako nimekulia nilitoka kwetu nikafikia Yemeke lakini mimi ni mwenyeji wa Kigoma.”

Licha ya kuanza na moto wa kufunga magoli mawili Rashid amesema hana ndoto za kuwa mfungaji bora wa mashindano kwa sababu anaondoka kwenda kambini kuungana na timu ya vijana ya Simba ambayo ipo mkoani Dodoma ikendele na mashindano ya U20.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here